Header Ads Widget

WAZEE WASTAAFU WALIA NA WAKE ZAO WANAOLALA NA NGUO, KUWANYIMA UNYUMBA


Baadhi ya viongozi  wa UWT Mkoa wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kikao cha tathimini kuisha

Suzy Luhende, Shinyanga press blog

Katibu wa Umoja wa Wanawake UWT Mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala amewataka madiwani wa viti maalumu, madiwani wanawake wa kata, wenyeviti na makatibu wa UWT wilaya kwenda kuzungumza na wanawake waache kulala na nguo, kwani kufanya hivyo ni kuwanyanyapaa wazee wastaafu kwa kuwanyima unyumba.

Hayo ameyasema leo kwenye kikao cha tathimini ya ugeni wa mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda, kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya CCM  Mkoa ambapo amewaomba viongozi hao wakazungumze na wanawake katika maeneo yao ili wanawake waweze kubadilika na kuwa na upendo na waume zao waache kuwanyanyapaa.

Kitandala amesema ametoa agizo hilo baada ya viongozi wa wazee wastaafu kwenda kutoa malalamiko na kumuomba kila kikao cha wanawake kitakachofanyika wanawake wakumbushwe kuacha kuwanyanyapaa waume zao kwa kulala na nguo kwa kisingizio kwamba wao ni wazee.

"Hivi karibuni nilikuwa ofisini kwangu wakaja mwenyekiti wa wazee na katibu wake kutoa malalamiko ya wazee wasitaafu wanadai  kwamba wazee wengi wastaafu wananyanyapaliwa kwa kunyimwa unyumba na wake zao ikiwemo watoto wao kuhodhiwa na wakina mama, watoto wamekuwa hawawapigii hata simu baba zao wanawajali mama zao tu,"amesema Kitandala.

"Mzee huyo kwa masikitiko alisema watoto wao wanawasomesha kwa nguvu kubwa, lakini wanapopata kazi wanawajua mama zao pekee wanapopiga simu wanaongea na mama zao na kuuliza baba yupo na ukibahatisha kuongea nae ni kukusalimia tu na kukata simu, hali ambayo inawafanya waumie na kupata stress na wengine kupoteza maisha "amesema Katibu.

"Mmoja wa wazee alisema sisi tunastaafu tukiwa na umri wa miaka sitini sio kwamba hatuwezi kufanya tendo la ndoa wakati mwingine tunaweza,kama asipolala na nguo hata nikiweka mkono tu katika mwili wake nitalidhika na kuwa na amani lakini anapolala na nguo ananifanya na kuwa na mawazo mengi ka wakati na huku ninamke wangu hivyo naomba uwaambie wanawake wabadilike ili wazee waweze kuishi wasifariki kabla ya muda wao,"amesema Kitandala

Akizungumza na viongozi hao Kitandala amewataka wanawake kila wanapofanya mikutano yao wawaombe wanawake wabadilike wasilale na nguo na wawe na upendo wa kwanza kwa waume zao wasiwanyanyapae kwani kufanya hivyo wanasababisha kuongezeka kwa vifo vya wazee pia wanawake wazungumze na watoto wao wawe wanaongea vizuri na baba zao ili waendelee kuishi.

"Wazee hao wamesema, wazee wengi wamekuwa wakiripotiwa wamebaka ni kwa sababu ya kunyimwa unyumba na mke wake ndiyo maana matukio mengi ya wazee yanatokea.

Aidha katibu huyo alimshukuru mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kwa kutoa michango mbalimbali kwa ajili ya wageni wa kitaifa hivyo aliwataka waendelee na moyo huo wa ushirikiano,na aliwapongeza wabunge wote wa mkoa wa Shinyanga hasa Ahamed Salumu ambaye alijitoa kwa wilaya tatu na Mkoa katika kuhakikisha wageni hawapati shida.

Pia aliwataka wanawake washirikiane na wabunge wote wa viti maalumu wasiwabague kwa sababu wanatoa ushirikiano wote kwa pamoja hivyo wawapende na pale wanapowahitaji katika shughuli mbalimbali wawashirikishe kwa pamoja kwani ukiwepo umoja kazi mbalimbali za jumuiya zinafanikiwa.

Kitandala aliwaomba viongozi hao waendelee kumuunga Mkono Rais Samia kwa kazi anazozifanya kwani anafanya maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, afya, maji, barabara, na umeme.

pia amewataka madiwani hao waende wakawasaidie kina mama  kupata mikopo ili waweze kujiimalisha kiuchumi kwani Rais ametoa fedha kwa ajili ya mikopo binafsi  kinachotakiwa ni kuwasimamia tu ili wapate mikopo hiyo.

Nao wazazi wametakiwa kukaa na watoto wao wa kike na kuwazuia wasivae nguo fupi yaani nusu uchi kwani kuvaa hivyo si maadili ya kitanzania, badalayake wavae nguo ndefu ambazo zinaficha maungo ya ndani ambayo hayatakiwi kuonekana hadharani.

Kwa upande wake kaimu mwenyekiti Christina Gule ambaye pia ni mjumbe wa baraza UWT Mkoa aliwashukuru viongozi wote waliojitoa kwenye ujio wa ugeni wa kitaifa pamoja na wanawake wafanyabiashara wa Shinyanga mjini kwa kujitoa kwa michango yao kwa ajili ya ugeni huo.
Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala akiwa akizungumza kwenye kikao cha tathimini

Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala akiwa akizungumza kwenye kikao cha tathimini
Mjumbe wa baraza la UWT Mkoa Christina Gule ambaye ambaye alisimama kama kaimu mwenyekiti wa Mkoa
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanili akizungumza kwenye kikao cha tathimini
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga akizungumza
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kahama akizungumza kwenye kikao cha tathimini
Diwani wa kata ya Bugharama wilayani Kahama akizungumza kwenye kikao cha tathimini

Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Flora akizungumza kwenye kikao cha tathimini

Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga Zamda Shaban akizungumza kwenye kikao cha tathimini
Diwani viti maalumu akichangia hoja
Wajumbe wa kikao hicho wakiendelea kuchangia hoja

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha tathimini
Baadhi ya viongozi wa wa UWT Mkoa wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kikao cha tathimini kuisha

Baadhi ya viongozi wa wa UWT Mkoa wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kikao cha tathimini kuisha
Baadhi ya viongozi wa wa UWT Mkoa wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kikao cha tathimini kuisha

Baadhi ya viongozi wa wa UWT Mkoa wakiwa kwenye picha ya pamoja madiwani wa Kishapu baada ya kikao cha tathimini kuisha
Baadhi ya viongozi wa wa UWT Mkoa wakiwa kwenye picha ya pamoja na madiwani wa halmashauri ya Shinyanga baada ya kikao cha tathimini kuisha
Baadhi ya viongozi wa wa UWT Mkoa wakiwa kwenye picha ya pamoja madiwani wa wilaya ya Kahama baada ya kikao cha tathimini kuisha

Kikao cha Tathimini kikiendelea
Kikao cha Tathimini kikiendelea
Kikao cha Tathimini kikiendelea







Post a Comment

0 Comments