Ofisa Maendeleo ya jamii Tedson Ngwale.
Na Kareny Masasy,Shinyanga
WADAU zaidi ya 150 mkoani Shinyanga wamepokea program Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) huku wakielezwa sayansi ya makuzi inayoambatana katika nguzo tano za lishe,ulinzi na usalama, ,afya,malezi yenye mwitikio na ujifunzaji wa awali.
Wadau hao leo tarehe 20/09/2023 baada ya kushiriki uzinduzi wa programu hiyo mkoani Shinyanga wamepewa elimu juu ya sayansi ya Makuzi na Malezi ya mtoto kutoka kwa mtaalamu Andrew Nkunga anayetokea kwenye Mtandao wa malezi na Makuzi ya Mtoto nchini (TECDEN).
Nkunga akitoa elimu hiyo amesema mtoto hatua za makuzi zinaanzia umri wa 0 hadi miaka nane ni kipindi ambacho mtoto ubongo unaanza kukua ikiwa atapata changamoto kwenye ukuaji hata ukuaji wake hautakuwa timilifu.
“Ubongo lazima ukue vizuri ili vitu vyote viende sawa na taarifa kupitia kwa mtoto kabla ya kuzaliwa na baada ya kuzaliwa hutumia milango ya fahamu na kupeleka kwenye ubongo hivyo wazazi na walezi wanashauriwa kutowatendea vitendo vya ukatili watoto,kuwatukana kuwafokea”amesema Nkunga.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amesema amepongeza wadau walioshiriki program jumuishi ikiwa inahitaji kupewa kipaumbele na watoto wote wawe katika ukuaji timilifu.
“Tumeelezwa hapa duniani kuna watoto taribani Millioni 250 wenye umri chini ya miaka mitano ambao wanapatikana kwenye nchi za uchumi wa kati na uchumi wa chini hivyo ni jukumu letu sote kuwalinda watoto ili wasipatwe na vitendo vya ukatili na kukua kwa utimilifu”.amesema mkude.
Afisa Maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale amesema taasisi zinazolea watoto ndani ya mkoa zinapatiwa mafunzo sababu zimekuwa zikiishi na watoto wenye umri mdogo kwa kusaidia wazazi wao ili watoto hao wawe katika msingi bora ambapo elimu inayotolewa sasa ni fursa ya namna ya kuwalea watoto ili kupata taifa imara.
Akitambulisha program hiyo kwa niaba ya mkurugenzi wa shirika la ICS Sabrina Majikata amesema kwanini wanazungumzia kuhusu umri wa miaka 0 hadi nane ni kumjenga mtoto katika ukuaji wake.
Majikata amesema mtoto akiwa bado mdogo ubongo unahitaji kujijenga zaidi na kunatakiwa kutiliwe mkazo katika nguzo tano za lishe,afyabora,Malezi yenye mwitikio,ujifunzaji wa awali na ulinzi na usalama.
“Serikali ilianza mchakato wa malezi na makuzi tangu mwaka 2004 na mwaka 2006 ilifanya mapatio ya sera ya mtoto na imeanza kupitiwa upya na viongozi hapa nchini kupitia sekta mbalimbali wametoa ahadi ya kutekeleza mchakato na sasa umeanza utekelezaji wake ili kumkomboa mtoto”amesema Majikata.
Majikata amesema shirika la watoto duniani (Unicef ) na shirika la afya duniani (WHO) lilitengeneza framu ya nguzo tano hizo kuhakikisha wanawekeza katika umri wa miaka mitatu lakini taifa la Tanzania liliangalia hilo nakuona kuwekeza katika umri wa mwaka 0 hadi nane.
“Wataalamu wanasema ukiwekeza katika umri mdogo ndiyo utaweza kumsadia mtoto katika ukuaji wake kwenye ubongo na sio kuwekeza katika umri mkubwa ubongo umekwisha komaa”anasema Majikata.
Mwakilishi wa meneja wa kanda ya ziwa kutoka Shirika la kimataifa la Word division Ngasa Michael amesema wanagusa watoto kupitia nguzo nne za ustawi wa mtoto ambao ni Afya, Elimu,Malezi na ulinzi na usalama kuhakikisha mtoto anakuwa katika ustawi ulio bora.
Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto mkoani Shinyanga akijitambulisha kwenye uzinduzi.
Wadau wakisikiliza mada ya elimu juu ya sayansi ya makuzi kwa mtoto.
Mtaalamu kutoka TECDEN andrew Nkunga akijitambulisha kwa wadau mkoani Shinyanga.
Mwakilishi wa shirika la ICS Sabrina Majikata akijitambulisha
Mwakilishi wa shirika la Doctors with Afrika akifuatilia mada.
Wadau wakifuatilia mada inayofundishwa baada ya uzinduzi wa programu jumuishi .
Wadau wakifuatilia elimu inayotolewa juu ya makuzi,maendeleo ya awali ya mtoto na malezi ya watoto
Mratibu wa WFT kutoka Shinyanga Gloria Mbia akijitambulisha kwa wadau wengine katika uzinduzi
Wadau wakisikiliza mada.