Na Kareny Masasy,
Kahama
Mashindano ya Ndondo Cup ambayo yanashirikisha vilabu vya timu za mpira wa miguu mitaani yanatarajia kuanza Mosi Oktoba mwaka 2023 wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa kushirikisha timu 16 zitakazo jitokeza kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa.
Akiongea na waandishi wa habari leo mratibu wa mashindano hayo Yahaya Mohamed Maarufu Mkazuzu ambayo pia yanadhaminiwa na clouds amesema lengo la kutaka timu hizo ni kunyanyua vipaji wakiamini vinaanzia huko na vimekosa kuonekana au kuendelezwa.
Mohamed amesema mpaka Sasa Kuna vilabu vimejisajili kushiriki mashindano hayo kwa mkoa wa Shinyanga na mwisho wa kuomba kushiriki mashindano hayo ni tarehe 22, Septemba,2023 huku akitaka viongozi wa vilabu vya mpira wa miguu wajitokeze.
"Mashindano haya kwa Sasa yamefikisha miaka kumi tangu kuanza kwake na yapo wazi kwa kila klabu kushiriki na kanuni za mpira ziko pale pale na mshindi atazawadiwa sh Millioni tano na mshindi wa pili sh Millioni tatu na hakuna mshindi wa tatu"amesema Mohamed.
Mohamed amesema mashindano hayo katika maeneo yaliyofanyika yamekuwa na mvuto wa hali ya juu ambapo Mashabiki wa timu watakao fanya vizuri katika ushangiliaji nao watapata zawadi na mshindi mmoja mmoja katika klabu aliyecheza atapata laki mbili na wachezaji watapewa jezi.
Katibu wa shirikisho la mpira wa miguu mkoa wa Shinyanga (SHIREFA)Marco Kaijage amesema vilabu vijitokeze visikatishe tamaa waratibu ,wameamua kuyachezea wilaya ya Kahama sio kwamba vilabu vya Kahama pekee bali yanahitaji vilabu vyote vilivyopo ndani ya mkoa huu.
Mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa miguu wilaya ya Kahama (KDFA) Hussein Salum amesema vilabu vya mpira wa miguu vijitokeze nani fursa kujitangaza na vilabu tisa vilivyojitokeza vingine vilikuwa vikisita kujisajili kwa kuwa na hofu huenda hayatakuwepo lakini leo mratibu amejitokeza Kahama vitazidi hitaji ya vilabu 16.
Kocha mkuu Frank Itohoro kutoka Mnarani Fc yenye Makazi yake kata ya Mhongolo amesema ni fursa kubwa kuja kwa Ndondo Cup kwani vijana wataonyesha vipaji vyao nakujitangaza wanaweza.
Kocha mkuu Shabani Ngogo kutoka Mbulu Fc yenye Makazi yake kata ya Nyasubi amesema mashindano hayo wameyasikia muda mrefu lakini mwaka huu yameletwa wilaya ya Kahama wameyapokea na maandalizi wameanza kuyafanya.
0 Comments