Header Ads Widget

DED KISHAPU AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI YA MVUA ZA EL-NINO

DED KISHAPU AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO

NA Ofisi ya Habari,KISHAPU

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Ndugu Emmanuel Johnson Mewataka Wananchi kuchukua Tahadhari ya Mvua za El-Nino kutokana na taarifa za Mamlaka ya Hari ya hewa nchi yetu inatarajia kupata Mvua za Eliminyo kwa hiyo ni vizuri kila Mwananchi kuchukua tahadhari.

Emmanuel Johnson ameyasema hayo tarehe 29 Septemba 2023 akiwa anafungua kikao cha Tathimini ya kilimo cha zao la Pamba kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.

Awali Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt Sabinus Chaula akiwasilisha taarifa ya Tathimini ya zao la Pamba ameeleza mafanikio Makubwa ya Zao la Pamba Wilaya ya Kishapu kwa Misimu Miwili,

"Mkoa mzima wa Shinyanga kwa msimu uliopita umezalisha Kilo Millioni 21, Kilo Millioni 17.4 Zimetoka Kishapu ni sawa na Asilimia 81 ya Pamba yote inatoka Kishapu. Licha ya Kuwa na Mafanikio Kuna Changamoto ambalo linaathiri zao la Pamba ni Pamoja na mabadiliko ya hari ya hewa." Amesema Dkt Chaula

Kwa upande wake Shija Mwandu Mkazinwa Kijiji cha Ikonda ameiomba Serikali kusimamia vizuri katika swala Zima la bei ya pamba kutoka na kubadilika Mara kwa Mara

"Kwa kweli tunaiomba Serikali kuangalia Swala la bei ya kununulia Pamba, Pamba inapokuwa nyingi tu bei inashuka hii inatuvunja moyo sisi wakulima wa Pamba kwa hiyo wito wangu kwa Serikali ni kuhakikisha wanasimamia vyema ilinituhamasishe zaidi" alizungumza Shija

Naye Meneja wa Redeso Ndugu Charles Buregeya amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yapo kwa hiyo amewaomba wanachi pia kulima mazao ya chakula ambayo yanahimili ukame pamoja kilimo cha Mkonge.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji Emmanuel Johnson Amewaagiza Maafisa Ugani kwenda kuwaelimisha Wakulima wajisajili kwaajili ya kutumia fursa ya Serikali kupewa ruzuku za mbolea na vinyunyizi.

Post a Comment

0 Comments