Header Ads Widget

HALMASHAURI YA MSALALA YAJIVUNIA KUONGEZA MAPATO NA KUVUKA LENGO.


Na Kareny  Masasy, Msalala

Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeendelea kujivunia kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato na kupata hati safi.

Hayo yamesemwa leo tarehe 25/07/2025  na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Khamis Katimba kwenye kikao cha  baraza la madiwani cha robo nne ya mwaka  huku kikiwa na ajenda ya kufanya uchaguzi wa kumpata makamu mwenyekiti na  wajumbe wa kamati mbalimbali.

Katimba amesema ukusanyaji wa mapato utaendelea kusimamiwa vizuri na  chama cha Mapinduzi kilimpatia  barua yenye jina moja la Mgombea  nafasi ya makamu mwenyekiti ambaye ni Flora Sagasaga na leo atapigiwa kura kwa kumthibitisha rasmi.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo  Mibako Mabubu  ambaye ameongoza zoezi la kupiga kura  kumpata makamu mwenyekiti  amesema waliopiga kura ni madiwani 22 na madiwani wanne hawakuhudhuria  baada ya kuomba ruhusa.

Mibako Mabubu aliwataja baadhi ya wenyeviti waliochaguliwa kwenye kamati ambapo kamati ya uchumi,ujenzi na  mazingira  amechaguliwa Ibrahimu Masanja,kamati ya Elimu,Afya na Maji amechaguliwa  Joseph Manyara na kamati mbili zimefanyiwa marekebisho ya wajumbe.

Flora Sagasaga ambaye amekuwa makamu mwenyekiti wa kuchaguliwa tena na madiwani wenzake  amesema  anawashukuru madiwani na chama kuendelea kumuamini zaidi  huku akiahidi kuendelea  kupokea ushauri.

Mbunge wa jimbo la Msalala Idd Kassim amesema  ukusanyaji wa mapato umekuwa mzuri amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu kwa kumleta mkurugenzi  Khamis Katimba ambaye naye amekuja kwa kasi kubwa kuhakikisha makusanyo ya fedha yanakwenda vizuri.

Mwenyekiti wa  Chama  Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama Thomas Muyonga amesifu  ukusanyaji wa mapato na kuvuka lengo huku akiwashukuru madiwani  kupiga kura bila kelele za kumrudisha makamu mwenyekiti kuongoza tena  nakukifanya chama kiendelee kuaminiwa zaidi.


Mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Mibako Mabubu akiongea kwenye kikao cha baraza la madiwani

Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala Khamis Katimba  akisikiliza hoja kwa umakini

Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Flora Sagasaga akiwashukuru madiwani wenzake kwa kumpigia kura na kushinda tena nafasi ya makamu mwenyekiti

Post a Comment

0 Comments