Header Ads Widget

WAZAZI WATAKIWA KUCHANGIA CHAKULA MASHULENI ILI KUONGEZA UFAULU


Diwani wa kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga Victor Mkwizu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara

Suzy Luhende, Shinyanga Press Blog

Diwani wa kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga Victor Mkwizu amefanya mkutano wa hadhara kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga, ili ziweze kutatuliwa kwa wakati, ikiwa ni pamoja na kuwataka wazazi kuishika mkono serikali kwa kuchangia fedha ya chakula ili kuongeza ufaulu mashuleni.

Mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Jasco kata ya Ngokolo, ambapo baadhi ya wananchi wametoa kero zao mbalimbali na kusikilizwa, diwani aliahidi kuzishughulikia kwa wakati ili waendelee na shughuli za kimaendeleo.

Akizungumza kwenye mkutano huo Mkwizu amesema wakati akigombea nafasi ya udiwani aliwaahidi wananchi kuwa atashughulikia kero zao mbalimbali na kuzipeleka sehemu husika kwa ajili ya kutatuliwa, pamoja na kusimamia miradi ya kimaendeleo katika kata yake na tayari kazi hiyo ameshaianza ili wananchi wake waishi kwa amani.

"Wakati nagombea nafasi hii niliahidi kutatua kero mbalimbali na kuwaletea miradi mbalimbali za kimaendeleo na sasa nimeanza kufanya mikutano kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi na kueleza mafanikio yaloyofanyika na yanayoendelea katika kata yetu ya Ngokolo,"amesema Mkwizu.

Amesema kuna miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa soko la kisasa katika kata hiyo, ambao kufikia mwezi wa sita utazinduliwa rasmi ili wananchi waendelee kufanya biashara mbalimbali na kujipatia kipato,pia kuna barabara nyingi zinaendelea kutengenezwa kwa kuwekewa vifusi na madaraja na serikali inampango wa kujenga kituo cha afya katika kata hiyo, ili wananchi wasiendelee kwenda kutibiwa mbali na ujenzi wake utaanza mapema June 2023.

Aidha amewataka wakazi wa kata hiyo kuendelea kukemea masuala ya ukatili wa kijinsia na kuwashauri wawe mabalozi wakutoa taarifa ili hatua ziweze kuchukuliwa na kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake kwa ajili ya kutokomeza ukatili na kukemea mmomonyoko wa maadili.

"Pia wakati tunaomba kura tuliahidi kwamba tunatokomeza ziro katika shele yetu ya sekondari Ngokolo na kweli tumetokomeza, shule yetu kwa mwaka 2022 haikuwa na ziro kabisa, ilikuwa na ufaulu wa asilimia 100 na sasa tunampango wa kutokomeza kabisa For, hivyo tuwaombe wazazi waishike mkono serikali wachangie chakula ili watoto hao wakipata chakula mashuleni wataweza kufaulu vizuri"amesema Mkwizu.

Naye afisa mtendaji wa kata ya Ngokolo Joshua Michael akisoma taarifa yake mbele ya Diwani amesema shule ya msingi Mwadui ina wanafunzi 16600, wanaokula chakula ni 600 hivyo wazazi waendelee kuchangia ili watoto wote waweze kula chakula shuleni.

Afisa maendeleo wa manispaa ya Shinyanga John Tesha amesema kata ya Ngokolo imependelewa kwa kuwa na miradi mingi kwa kutumia mapato ya ndani ina soko ambalo limetumia fedha nyingi ambao litabeba wafanyabiashara wote wanaouza mitumba .

"Lengo letu ni moja kujenga manispaa yetu, hivyo niwaombe ushirikiano wenu ili tufanye maendeleo makubwa zaidi, ili manispaa yetu iendelee kuwa safi tuendelee kuchangia fedha za usafi ili uchafu uchukuliwe upelekwe kwenye Dampo, pia katika kata ya Ngokolo manispaa imetoa mkopo Sh 150 milioni kwa vikundi mbalimbali vilivyopo,"amesema Tesha.

"Labda naomba ni waeleweshe huo ni mkopo sio Ruzuku, ukichukua lazima ulejeshe, na kama ulichukua kiujanja ujanja ukakimbia utakamatwa tu, dawa ya deni ni kulipa mkono wa serikali ni mrefu sana ukijifichwa utakamatwa tu,ameongeza 

Katibu wa Jumuiya ya vijana Naibu Katalambula ambaye alimwakilisha katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Ally Majeshi amesema kata ya Ngokolo ina miradi mingi ambao jumla ya fedha zaidi ya bilioni 1 imemwagwa kwa ajili ya maendeleo, hivyo amewataka wananchi wasimamie na kuwahimiza watoto kwenda shule na kukemea ndoa za utotoni na mimba za utotoni.


Baadhi ya wananchi wa mitaa mbalimbali walitoa kero zao akiwemo Elizabeth Piter ambaye aliuliza swali kwamba ni lini walengwa wa Tasaf watalipwa fedha yao, ambapo waliahidiwa kuwa kero zao zote zitafanyiwa kazi kwa wakati.
Diwani wa kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga Victor Mkwizu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara

Diwani wa kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga Victor Mkwizu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara


Diwani wa kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga Victor Mkwizu akiwa kwenye mkutano wa hadhara akisaini ili aanze kuhutubia

Katibu wa Jumuiya ya vijana Uvccm wilaya ya Shinyanga Naibu Katalambula akizungumza kwenye mkutano wa hadhara

Afisa maendeleo wa manispaa ya Shinyanga John Tesha akizungumza kwenye mkutano wa hadhara

Afisa mtendaji wa kata ya Ngokolo Joshua Michael akisoma taarifa ya kata hoyo
Mwenyekiti wa mtaa wa Kalonga akizungumza kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa CCM kata ya Ngokolo George Mwandu akizungumza kwenye mkutano huo
Katibu wa chama cha Mapinduzi CCM kata ya Ngokolo Kichele akizungumza
Mwenyekiti wa mtaa wa Mageuzi Erick Elias akizungumza kwenye mkutano wa hadhara


Mwenyekiti wa mtaa wa Mwadui Mwalimu Nuru akizungumza kwenye mkutano huo
Kazi iliendelea katika viwanja vya Jasco

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT kata ya Ngokolo Hulda Nasoro mwenye ushungi akiwa kwenye mkutano huo
Viongozi wa Chama na serikali wakiwa kwenye kikao

Viongozi wa mitaa wakifuatilia kwa umakini

Wananchi wa kata ya Ngokolo wakiwa kwenye mkutano huo

Wananchi wa kata ya Ngokolo wakiwa kwenye mkutano huo

Wananchi wa kata ya Ngokolo wakiwa kwenye mkutano huo

Kazi inaendelea kwa wananchi wakiuliza maswali ya papo kwa papo

Enginear Maige kutoka Tarura akijibu maswali ya wananchi

Mzee wa baraza Sylivester Senga akiwataka wazee wote wa ngokolo wajiandikishe ili wapate huduma zao stahiki

Maswali yakiendelea

Wananchi wakiuliza maswali ya papo kwa papo

Wananchi wakiuliza maswali ya papo kwa papo
Wananchi wakiuliza maswali ya papo kwa papo
Kila mtu alikuwa akitafakari baada ya kusikia taarifa ya maendeleo ya kata hiyo ambapo wengine waliishukuru serikali kwa kazi kubwa ya maendeleo iliyofanyika katika kata ya NgokoloPost a Comment

0 Comments