Header Ads Widget

TAKUKURU YABAINI MIANYA YA RUSHWA KATIKA MFUMO WA UTOAJI MBOLEA NA UENDESHAJI WA MASOKO -SHINYANGA.

 TAKUKURU YABAINI MIANYA YA RUSHWA KATIKA MFUMO WA UTOAJI MBOLEA NA UENDESHAJI WA MASOKO -SHINYANGA.

Na mwandishi wetu.

Takukuru mkoa wa Shinyanga yabaini mapungufu na uwepo wa mianya ya rushwa katika mfumo wa utoaji wa pembejeo katika wilaya ya kahama na mfumo wa uendeshaji wa masoko katika wilaya ya  Kishapu.Takukuru imebani dosari hizo baadaya kufanya uchambuzi wa mifumo kwa halmashauri za hizo kwa kipindi cha januari hadi machi 2023.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga,Donasian Kessy ameeleza hayo leo mei 25,2023 katika vyombo vya habari mkoani shianyanga,wakati akiwasilisha taarifa ya robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/2023(Januari hadi machi 2023) juu ya uthibiti wa vitendo vya rushwa mkoani shinyanga.

Kessy anasema,Takukuru ilifanya uchambuzi wa mifumo katika halmashauiri ya wilaya ya Kahama na Kishapu ili kuweza kuziba mianya ya rushwa ,ambapo walibaini mapungufu katika utoaji wa pembejeo kwa kata zongomera,busoka na mwendakulima za wilaya ya Kahama  na dosari ya uendeshaji wa soko la maganzo wilaya ya Kishapu.

“Vitabu vya usajili havirudishwi kwa wakati vituoni,kwani wakulima bado wanahitaji kujiandikisha na hata waliojiandikisha hawapati mrejesho wowote au namna ya siri ili kwenda kuchukua mbolea na baadhi ya wakulima kusajiliwa Zaidi ya mara moja kwenye mfumo wa kuandaliwa namba ya siri tofauti ,mfano kijiji cha zongomela baadhi ya wakulima waliandikishwa mara mbili”anasema Kessy

kukosekana kwa rejesta inayoonesha idadi ya wafanyabiashara kwa kila soko na rejesta ya fremu zinazozunguka soko la maganzo” Anasema kessy.

Kwa upande mwingine,Takukuru walipokea malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya taasisi ndogo za fedha kukataa kutoa salio la deni analodaiwa mteja pindi anapoomba salio la deni lake.

Malalamiko mengi yalihusu benki ya ABC tawi la Kahama ambapo ofisi iliingilia kati na benki hiyo kutoa taarifa za salio la deni kwa wahusika”anasema kessy

Katika hatua nyingine,Takukuru ilifatilia miradi ya maendeleo arobaini na nne(44) yenye thamani ya Tshs bilion 5.1  na kubaini mapungufu katika miradi miwili(2) yenye thamani ya tshs million 86 ambapo mradi wa vyumba viwili vya madarasa katika sekondari ya bunambiyu wenye thamani ya tshs million 40 na ujenzi wa madarasa mawili yenye thamani ya tshs milioni 46 ya shule ya sekondari ikonda.

Katika shule ya sekondari bunambiyu,jengo kutosimikwa vizuri kwenye kuta pamoja na dari,kopo za madirisha kupinda,madirisha ya aluminium kutokwekwa vizuri na badaya yake kukandikwa na sementi nyeupe,kuwepo na nyufa kwenye baadhi ya madirisha na mikanda ya bodi kuachia nyufa

Kwa upande wa shule ya sekondari ikonda,mzabuni alilipwa tshs million 5 tangu julai 2022 na hakuwahi kupelekea vifaa vya ujenzi”anasema kessy.


Post a Comment

0 Comments