Header Ads Widget

MISA-TANZANIA YATAJA MAFANIKIO YA MIAKA 30 TANGU KUANZISHWA KWAKE, SERIKALI YAAHIDI KUFANYIA MAREKEBISHO SHERIA HUDUMA YA HABARI

Maadhimisho ya miaka 30 ya Misa-Tanzania.

Na Marco Maduhu, DODOMA

TAASISI ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA Tanzania), imeadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993, huku yakitajwa mafaniko ambayo imeyafanya katika Tasnia ya habari ndani ya miaka hiyo.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Mei 25, 2023 Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari, pamoja na wanachama wa Misa Tanzania, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa kwa niaba ya Waziri wa habari na Teknolojia na Mawasiliano Nape Nnauye.

Msigwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa Misa Tanzania, amesema Serikali chini ya Rais Samia inatambua kazi nzuri ambayo inafanywa na waandishi wa habari katika kuhabarisha umma, na kutangaza mambo mazuri ya kimaendeleo ambayo inayatekeleza.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya habari Teknolojia na Mawasiliano itaendelea kushirikiana vyema na waandishi wa habari katika kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili, pamoja na kutekeleza Maagizo ya Rais Samia ya kuifanyia Marekebisho ya Sheria ya huduma za habari ya mwaka (2016) kwa kurekebisha vifungu ambavyo vinabinya uhuru wa habari na kujieleza.

“Serikali chini ya Rais Samia ipo bega kwa bega na Waandishi wa habari na ndiyo maana ndani ya miaka miwili ya utawala wake hamjasikia chombo chochote cha habari ambacho kimefungiwa, na Magazeti ambayo yalifungiwa yalifunguliwa lesseni zao,”amesema Msigwa.

“Serikali pia imepunguza Tozo kwa vyombo vya habari vya mtandaoni (Online) kutoka ulipaji wa lesseni kutoka Sh.100,000 hadi 50,000, ulipaji Ada kwa mwaka mzima ilikuwa Sh.Milioni Moja na sasa Sh. Laki Tano, yote haya ni kuonyesha jinsi gani Serikali ipo pamoja na Waandishi wa habari,”ameongeza.

Katika hatua nyingine ametoa Rai kwa Waandishi wa habari kujiendelea kielimu, pamoja na Taasisi mbalimbali za habari kuendelea kutoa mafunzo zaidi kwa wana Tasnia hao, ili wawe wanafanya kazi zao kwa weledi, kuzingatia maadili ya habari na sheria za habari.

Naye Mwenyekiti wa Misa-Tanzania Salome Kitomari, akisoma taarifa kwenye maadhimisho hayo, ametaja mafanikio mbalimbali ambayo yamepatikana ndani ya miaka 30 ya Misa-Tan, kwamba ni kuwezesha uanzishwaji wa vyombo vingine vya habari zikiwamo Radio za kijamii.

Ametaja Mafanikio mengine kuwa wamefanya uragibishi kwenye sheria mbalimbali tangu Sheria ya Magazeti, Sheria ya Huduma za Habari, Sheria ya Haki ya Taarifa na nyinginezo, pia imefanya mafunzo nchi nzima kuwajengea uwezo waandishi kuzijua sheria zinazosimamia taaluma, na kuandika habari za jinsia na COVID-19.

Pia mafanikio mengine ni upatikanaji wa taarifa kwa kusukuma kuwa na sheria ya haki ya Taarifa, 2016, na kuongeza msukumo wa utoaji wa taarifa.

“Mathalani, kila mwaka Septemba 28, ambayo ni siku ya Haki ya Taarifa, MISA hutoa ripoti ya utafiti kuonyesha wale waliofanyiwa utafiti kwa kiasi gani walitoa taarifa.kwa ujumla kuna mabadiliko siku hadi siku, pia kukutana na wabunge, na viongozi wa serikali,”amesema Kitomari.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Misa-Tanzania Elizabeth Riziki, amesema MISA ilianzishwa mwaka 1993, baada ya kikao cha wanahabari waliokutana Windhoek, Namibia kujadili mambo mbalimbali yaliyokuwa yanaukabili Ukanda wa Nchi za Kusini.

Amesema kwa mwaka huu 2023, MISA Tanzania inaazimisha miaka 30, kwakufanya kazi ya kichechemuzi katika uhuru wa Habari, Uhuru wa kujieleza,kupata na kutoa taarifa.

Amesema katika maadhimisho hayo ambayo yachukua muda wa siku mbili, wadau watajadiliana kuhusu kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia na namna ambavyo umma unahusishwa kwenye uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa taarifa.

Majadiliano mengine ni changamoto zilizopo kwenye sekta ya habari na kuweka mkakati wa kuzitatua, ikiwamo namna ya kuboresha maisha ya waandishi wa habari.

Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ya Misa-Tanzania mwaka huu (2023) inasema “Uhuru wa kujieleza msingi wa haki kwa maendeleo endelevu.”
Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 30 ya Misa-Tanzania.
Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 30 ya Misa-Tanzania.
Mkurugenzi wa Misa-Tanzania Elizabeth Riziki akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa Misa-Tanzania.
Mwenyekiti wa Misa-Tanzania Salome Kitomari akizungumza kwenye Maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Uongozi Misa Kanda Dk. Tabani Moyo akizungumza kwenye Madhimisho hayo.
Mwakilishi wa Internews Agnes Kayuni akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 30 ya Misa-Tanzania.
Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Misa-Tanzania (katikati) Salome Kitomari na Mkurugenzi wa Misa-Tanzania Elizabert Riziki, kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya MISA.
Wanachama wa Misa-Tanzania wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa Taasisi hiyo.
Maadhimisho ya miaka 30 ya Misa-Tanzania yakiendelea.

Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikipigwa.

Post a Comment

0 Comments