Header Ads Widget

SHUWASA YAWAPA ZAWADI WADAU VINARA WA KUTOA TAARIFA ZA UVUJAJI MAJI, ULINZI WA MIUNDOMBINU


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akimpatia zawadi Mzee Zengo Mikomangwa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akionesha Tuzo ya ushindi kwa kupunguza upotevu wa maji ambapo mamlaka hiyo imekuwa Mamlaka ya kwanza katika kupunguza upotevu wa maji kwenye mamlaka za mikoa nchini katika mwaka 2021/2022.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imetoa zawadi kwa wadau walioongoza (vinara) kwa kutoa taarifa za uvujaji wa maji, ulinzi wa miundombinu ya maji na kuboresha huduma ya maji katika Manispaa ya Shinyanga na miji midogo ya Didia, Tinde na Iselamagazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.


Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa wadau hao leo Jumatatu Machi 27,2023, Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Mhandisi Yusuph Katopola amesema zawadi hizo ni sehemu ya kutambua mchango mkubwa unaotolewa na wadau kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga.


“SHUWASA inatambua kazi nzuri inayofanywa na wadau katika utoaji taarifa kuhusu taarifa za uvujaji wa maji, ulinzi wa miundombinu ya maji na kuboresha huduma ya maji kwa njia mbalimbali ikiwemo Mitandao ya kijamii (Magroup ya Whatsapp). Kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya maji mwaka huu, tunawapatia zawadi ya Notebook, miamvuli na nauli wadau hawa”, amesema Mhandisi Katopola.


“Wadau wa maji wa ndani na nje ya SHUWASA wamechangia kwa kiasi kikubwa SHUWASA kuibuka mshindi wa kwanza katika Mamlaka za Maji za mikoa nchi nzima kwa mwaka 2021/2022 ambapo hivi karibuni EWURA imetupa tuzo ya mamlaka ya Maji iliyoibuka kidedea kwa kupunguza upotevu wa maji. Tunawashukuru sana, endeleeni kutupatia taarifa na maoni kuhusu uboreshaji wa huduma za maji”, ameongeza Mhandisi Katopola.


Nao wadau waliopatiwa zawadi akiwemo Joseph Ndatala, Nalinga Najulwa na Zengo Mikomangwa wameishukuru SHUWASA kwa kutambua mchango wao katika utoaji taarifa za uvujaji wa maji na ulinzi wa miundombinu ya maji na maoni mbalimbali ya kuboresha huduma za maji.

Aidha wameipongeza SHUWASA kwa kupunguza malalamiko ya wananchi kuhusu huduma za maji hali inayotokana na uwajibikaji mzuri wa wafanyakazi wa SHUWASA.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akionesha Tuzo ya ushindi kwa kupunguza upotevu wa maji ambapo mamlaka hiyo imekuwa Mamlaka ya kwanza katika kupunguza upotevu wa maji kwenye mamlaka za mikoa nchini katika mwaka 2021/2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wadau walioongoza kwa kutoa taarifa za uvujaji wa maji, ulinzi wa miundombinu ya maji na kuboresha huduma ya maji katika Manispaa ya Shinyanga na miji midogo ya Didia, Tinde na Iselamagazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wadau waliongoza kwa kutoa taarifa za uvujaji wa maji, ulinzi wa miundombinu ya maji na kuboresha huduma ya maji katika Manispaa ya Shinyanga na miji midogo ya Didia, Tinde na Iselamagazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) , Nsianel Gelard akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wadau walioongoza kwa kutoa taarifa za uvujaji wa maji, ulinzi wa miundombinu ya maji na kuboresha huduma ya maji
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola (katikati aliyeshikilia tuzo) ,Afisa Uhusiano wa SHUWASA Nsianel Gelard (kulia) wakipiga picha ya kumbukumbu wadau walioongoza kwa kutoa taarifa za uvujaji wa maji, ulinzi wa miundombinu ya maji na kuboresha huduma ya maji katika Manispaa ya Shinyanga na miji midogo ya Didia, Tinde na Iselamagazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola (katikati aliyeshikilia tuzo), Afisa Uhusiano wa SHUWASA Nsianel Gelard (kulia) wakipiga picha ya kumbukumbu wadau walioongoza kwa kutoa taarifa za uvujaji wa maji, ulinzi wa miundombinu ya maji na kuboresha huduma ya maji katika Manispaa ya Shinyanga na miji midogo ya Didia, Tinde na Iselamagazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) , Nsianel Gelard akionesha mwamvuli ambao ni sehemu ya miamvuli waliyopatiwa wadau walioongoza kwa kutoa taarifa za uvujaji wa maji, ulinzi wa miundombinu ya maji na kuboresha huduma ya maji
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) , Nsianel Gelard akionesha note book ambayo ni sehemu ya note book walizopatiwa wadau walioongoza kwa kutoa taarifa za uvujaji wa maji, ulinzi wa miundombinu ya maji na kuboresha huduma ya maji
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akimpatia zawadi Fedrick Kimaro
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akimpatia zawadi Mzee Nalinga Najulwa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akimpatia zawadi Joseph Ndatala
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akimpatia zawadi Suleiman Abeid
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akimpatia zawadi Elias Kulwa
Zoezi la kukabidhi zawadi likiendelea
Zoezi la kukabidhi zawadi likiendelea
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akimpatia zawadi mfanyakazi wa SHUWASA, Zephania Kibona
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akimkabidhi zawadi mfanyakazi wa SHUWASA, Asela Moye
Zoezi la kukabidhi zawadi likiendelea
Zoezi la kukabidhi zawadi likiendelea
Mdau wa maji Zengo Mikomangwa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi
Mdau wa maji Najulwa Nalinga akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi
Mdau wa maji Joseph Ndatala akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi
Wafanyakazi wa SHUWASA wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wafanyakazi wa SHUWASA wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wafanyakazi wa SHUWASA wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wafanyakazi wa SHUWASA wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
   Wafanyakazi wa SHUWASA wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wafanyakazi wa SHUWASA wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola (katikati aliyeshikilia tuzo) ,Afisa Uhusiano wa SHUWASA Nsianel Gelard wakipiga picha ya kumbukumbu wadau walioongoza kwa kutoa taarifa za uvujaji wa maji, ulinzi wa miundombinu ya maji na kuboresha huduma ya maji.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola (katikati aliyeshikilia tuzo) ,Afisa Uhusiano wa SHUWASA Nsianel Gelard wakipiga picha ya kumbukumbu wadau walioongoza kwa kutoa taarifa za uvujaji wa maji, ulinzi wa miundombinu ya maji na kuboresha huduma ya maji.
Wafanyakazi wa SHUWASA na wadau wakipiga picha ya pamoja
Wafanyakazi wa SHUWASA na wadau wakipiga picha ya pamoja.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments