Header Ads Widget

MJUMBE WA BARAZA LA WAZAZI CCM TAIFA ATOA MSAADA KWA WAJAWAZITO, WAZAZI NA WAGONJWA WOTE WALIOKUWA WAMELAZWA KITUO CHA AFYA MWENDAKULIMA KAHAMA

Mjumbe wa baraza la Jumuiya ya wazazi CCM Taifa Edwin Nyakanyenge akizungumza kwenye kikao cha  viongozi wa chama na Jumuiya ya wazazi ngazi ya kata

Suzy Luhende, Shinyanga Blog

Mjumbe wa baraza la Jumuiya ya Wazazi Taifa CCM Edwin Nyakanyenge  ametoa msaada wa zaidi ya Shilingi 200,000 kwa wajawazito, wazazi na wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika kituo cha afya cha Mwendakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambazo zitawasaidia kununua chakula wakati wakiwa hospitalini hapo.

Nyakanyenge  ambaye aliambatana na mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Shinyanga John Siagi kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kuwajulia hali na kuzungumza na mesema Viongozi wa CCM ngazi ya kata, baada ya kuwaona wagonjwa hao amewiwa kutoa shilingi elfu tano tano (5000)kwa kila mgonjwa aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo, ambazo zitawasaidia kununua chakula. 

"Kwa kweli baada ya kufika hospitalini hapa kwa ajili ya kuona wagonjwa nimewiwa kuwasaidia kiasi hiki kidogo ambacho kitawasaidia kupata chakula kwa siku ya leo, hivyo nawaombea Mungu azibariki dawa wanazotumia na waliokuja kujifungua wsjifungue salama ili waweze kurejea majumbani kwao,"amesema Nyakanyenge.

"Na baada ya kufika hospitalini hapa wakati nikiwa kwenye ziara na mwenyekiti wangu wa wazazi nimekutana na mtoto ambaye ameletwa hospitalini hapa anaumwa, lakini baada ya kuuliza nimeambiwa ameletwa hapa na bibi yake, lakini mama yake alitelekeza akakimbia kusikojulikana,hivyo nimeahidi nitamletea chakula cha lishe ili aweze  kula na kurudisha mwili kwa sababu anaonekana amedumaa mwili kwa kutopata lishe ya chakula,"amesema Nyakanyenge.

"Kwa kweli inasikitisha sana mtoto ana mwaka mmoja anapewa ugari na nyanya chungu badala ya uji ni huruma sana mimi bajitolea kesho nitaleta chakula chake mpaka pale atakapokaa vizuri,lakini niwaombe wazazi hawa watoto mnaowazaa mnatakiwa msiwakimbie muwalee mpaka wakue ndiyo muende mkafanye shughuli zenu ukimuacha hivi ni mateso, angali bibi ana mtoto wake halafu kaachiwa mtoto mwingine jamani ni dhambi namuomba kokote aliko mzazi wa mtoto huyu arudi alee mtoto wake.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga ameahidi kumtumia nguo mtoto huyo ambaye ametelekezwa na mama yake na kuwataka wazazi kuwa na huruma na watoto wao, kwani wanapowaacha na kukimbilia kusikojulikana huku bibi yake akihangaika na chakula anachotakiwa kula hakipati ni mbaya sana.Mjumbe wa Baraza la Jumuiya ya wazazi Taifa Edwin Nyakanyenge akizungumza kwenye kikao cha viongozi wa chama na Jumuiya ya wazazi ngazi ya kataMjumbe wa Baraza la Jumuiya ya wazazi Taifa Edwin Nyakanyenge akisalimia mtoto aliyetelekezwa na mama yake


Mjumbe wa Baraza la Jumuiya ya wazaziTaifa Edwin Nyakanyenge

Mjumbe wa baraza la Jumuiya ya wazazi Taifa Edwin Nyakanyenge akitoa msaada kwa wagonjwa katika kituo cha afya Mwendakulima

Mjumbe wa barazala Jumuiya ya wazazi Taifa Edwin Nyakanyenge akitoa msaada kwa wagonjwa katika kituo cha afya Mwendakulima

Mjumbe  lawa baraza Jumuiya ya wazaziTaifa Edwin Nyakanyenge akitoa msaada kwa wagonjwa katika kituo cha afya Mwendakulima
Mjumbe  wa  baraza la Jumuiya ya wazazi Taifa Edwin Nyakanyenge akimjulia hali mtoto aliyetelekezwa na mama yake

Post a Comment

0 Comments