Header Ads Widget

BUNGE LA AFRIKA LAHAMASISHA MATUMIZI YA DAWA ZA ASILIMakamu wa Rais wa Pili wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) Mhe. Dkt. Ashebiri Gayo kutoka Ethiopia akizungumza leo Jumatano Machi 15,2023 wakati anafungua
Warsha ya Pamoja juu ya nafasi ya dawa za asili (Traditional medicine) katika mifumo ya afya ya Afrika iliyoshirikisha Wabunge wa Bunge la Afrika na Wadau mbalimbali wa afya katika Ukumbi wa Bunge la Afrika, Mdrand Afrika Kusini.
Dkt. Gayo amesema suala la dawa za asili linagusa uchumi hivyo kuna uhitaji mkubwa wa kukuza dawa za asili ili kuwezesha kuunganishwa kwake katika mifumo ya afya barani Afrika huku akiliomba Shirika la Afya Duniani (WHO) kushirikiana na Afrika pindi wanapogundua dawa  kwa matumizi mbalimbali badala ya kuweka vikwazo.


"Tunataka kukuza tiba asilia katika nchi zetu za Afrika ili kuchangia katika kuboresha huduma ya afya ya watu wetu lakini pia kuhakikisha nafasi ya dawa za asili katika mifumo ya afya inatambuliwa. Tunataka pia kuhakikisha dawa za asili zinaboreshwa kisasa lakini pia Sheria zinaimarishwa ili kudhibiti utafiti katika dawa za asili",amesema Dkt. Gayo.


Nao washiriki wa warsha hiyo wamesema WaAfrika wanatakiwa kuzipa kipaumbele dawa za asili na kuondokana na mitazamo hasi kwamba kutumia dawa za asili ni ushamba/uchawi/zimepitwa na wakati wakibainisha kuwa hata wakati wa janga na Covid - 19 dawa za asili zimesaidia sana kutibu afya za watu lakini pia dawa hizo zimekuwa zikitumiwa na mababu zetu hivyo ni vyema utamaduni ukaenziwa kwa kuwekewa nguvu zaidi pia kwenye Idara za Afya/Wizara za Afya katika nchi.

Aidha wameshauri Serikali za nchi za Afrika kuongeza Bajeti kwenye eneo la Tiba Asili kwani tiba asilia ni nzuri na ina gharama nafuu.
Makamu wa Rais wa Pili wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) Mhe. Dkt. Ashebiri Gayo kutoka Ethiopia akizungumza leo Jumatano Machi 15,2023 wakati anafungua
Warsha ya Pamoja juu ya nafasi ya dawa za asili (Traditional medicine) katika mifumo ya afya ya Afrika. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
 
Makamu wa Rais wa Pili wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) Mhe. Dkt. Ashebiri Gayo kutoka Ethiopia akizungumza leo Jumatano Machi 15,2023 wakati anafungua
Warsha ya Pamoja juu ya nafasi ya dawa za asili (Traditional medicine) katika mifumo ya afya ya Afrika
Dkt. Georges Ki Zerbo kutoka WHO akiwasilisha mada wakati wa warsha hiyo
Mtaalamu wa Tiba Asili  Rene Munya kutoka Afya Health Products (M- Power & Moringa) akiwasilisha mada wakati wa warsha hiyo

Post a Comment

0 Comments