Header Ads Widget

KITUO CHA TAARIFA NA MAARIFA WASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI SHINYANGA

Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa wilayani Kishapu Fredina Said (kushoto) akimuelezea Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude bidhaa mbalimbali ambazo wanazitengeneza za ujasiriamali kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga alipotembelea kwenye banda lao.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KITUO cha Taarifa na Maarifa Kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ambacho kipo chini ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wameshiriki kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani mkoani Shinyanga na kuonyesha bidhaa mbalimbali za ujasiriamali ambazo wanazitengeneza na kuwa kwamua kiuchumi.

Màdhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yamefanyika leo Machi 8,2023 katika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.

Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa wilayani Kishapu Fredina Said akizungumza wakati Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude alipotembelea banda lao, amesema wanakikundi wamekuwa wakijishughulisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kiuchumi yakiwamo mafuta ya kujipaka, Sabuni, Batiki, na Taulo za kike za kufua kwa ajili ya wanafunzi kujistili hedhi, vikiwamo na vitu mbalimbali vya urembo.

"Tumeanzisha shughuli hizi za uzalishaji mali ili wanawake wapate vipato na kuondokana na ukatili wa kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi kwa waume zao,"amesema Said.

Aidha, wametoa wito kwa wadau wa maendeleo ambao wanapenda kufadhili watoto Taulo za kike za kufua, wawa unge mkono na kuwasiliana nao ili wazitengeneze nyingi na kumuokoa mtoto wa kike asikose vipindi vya masomo wakati wa hedhi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, amewapongeza wanawake kwa kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali na kujikwamua kiuchumi, huku akiwataka waendelee kuchangamkia fursa ya mikopo ya Halmashauri asilimia 10 ambayo haina Riba.

Kauli Mbiu katika Maadhimisho hayo ni Ubinifu na Mabadiliko ya Teknolojia, chachu katika kuleta usawa wa kijinsia, huku Maadhimisho hayo yakihudhuliwa pia na Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa wilayani Kishapu Fredina Said (kushoto) akimuelezea Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude bidhaa mbalimbali ambazo wanazitengeneza za ujasiriamali kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga alipotembelea kwenye banda lao.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo (kulia) akinunua Asali bidhaa ambazo zinatengenezwa na wana kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Ukenyenge wiayani Kishapu, alipotembelea banda lao kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga.

Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi akiwa kwenye banda la kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu akiangalia bidhaa mbalimbali ambazo wanazitengeneza alipotembelea banda lao kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiwa kwenye banda la kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu akiangalia bidhaa mbalimbali ambazo wanazitengeneza alipotembelea banda lao kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga.

Wanakituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu wakipiga picha pamoja wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga.

Wanawake wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa wa Shinyanga Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Wanawake wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Post a Comment

0 Comments