Header Ads Widget

BARRICK YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTOA MSAADA WA VIFAA VYA MATIBABU HOSPITALI YA MWANANYAMALA


Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini ,Georgia Mutagahywa (wa tatu kushoto) akimkabidhi vifaa vya hospitali kwa Daktari wa hospitali ya Mwananyamala Eliyafie Huruma sehemu ya vifaa, vilivyotolewa na kampuni ya Barrick katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Barrick na hospitali ya Mwananyamala.
Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini ,Georgia Mutagahywa (wa tatu kushoto) akibadilishana mawazo na Katibu wa afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Lilian Mwanga baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya matibabu vilivyotolewa na Barrick katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Barrick na hospitali ya Mwananyamala.

******
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Wafanyakazi Wanawake wa kampuni ya Barrick kutoka ofisi ya Dar es Salaam wametembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala na kukabidhi vifaa mbalimbali vya kusaidia matibabu vilivyotolewana kampuni pia walipata fursa ya kutembelea wodi ya wazazi ya hospitali hiyo.

Akiongea na uongozi wa Hospitali hiyo, Meneja Mawasiliano wa Barrick Nchini (Corporate Communications and Country Liasion Manager) Georgia Mutagahywa, amesema katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu 2023, pamoja na kampuni kuwa na programu mbalimbali za ndani pia imeandaa programu za kusaidia jamii.

Amesema Barrick imekuwa ikitoa kipaumbele kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini ambapo kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii imeweza kujenga vituo vya afya katika maeneo yanaozunguka migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara.

Katibu wa Afya wa Hospitali hiyo,Lilian Mwanga ameishukuru Barrick kwa msaada huo sambamba na baadhi ya wafanyakazi wake kujitolea muda wao kutembelea hospitali na kutembelea wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo ikiwemo Wanawake waliolazwa katika wodi ya wazazi.

Post a Comment

0 Comments