Header Ads Widget

WAJUMBE WA EVAWC WG SHINYANGA WATAKIWA KUWA NA NGUVU MOJA KATIKA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA




Mwenyekiti wa Shinyanga Ending Violence Against Working Group  Shinyanga (EVAWC  WG) Jonathan Manyama akizungumza kwenye kikao cha robo mwaka kilichofanyika mjini Shinyanga

Suzy Luhende, Shinyanga Blog

MWENYEKITI wa Shinyanga Ending Violence Against Working Group  Shinyanga (EVAWC  WG) Jonathan Manyama amewataka wajumbe wa Working Group kushirikiana kwa pamoja katika kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Hayo amesema  leo   wakati akizungumza kwenye kikao cha robo mwaka wa Evawc uliofanyika mjini hapa, ambapo amewataka wajumbe wote kuwa na umoja na nguvu moja ili kuhakikisha wanatokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

"Niwaombe ndugu zangu tuone hiki chombo ni cha thamani sana tunapokutana tushirikiane kikamilifu wote kwa nguvu moja katika kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto,tukiwa pamoja na tufanye kazi zetu kwa amani ili kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto,"amesema Manyama.

"Lengo la group hili  ni kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, hivyo hatuko tayari kulea mtu ambaye yuko kinyume na sisi anatukosea heshima, tunataka mtu anaetoa ushirikiano wa kutokomeza ukatili, kwani kuna watoto wanafanyiwa ukatili na kuna wanawake wanafanyiwa ukatili tuwasaidie tuelimishe jamii iachane na ukatili wa aina yeyote,"amesema Manyama.

Kwa upande wake mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia amewataka waendelee kushirikiana katika kufanya kazi zao kwa amani kabisa  wasiwasikilze watu ambao wanaweza kuvuruga kikundi hicho.

"Endeleeni kujifunza na kuangalia wapi hamjafanya, wafikieni wananchi muwaelimishe waondokane na mila potofu ukatili kwa watoto na wanawake na mfanye kazi zenu kwa amani kabisa muendeleze nguvu ya pamoja ili kuhakikisha mnatokomeza ukatili wa kijinsia, kwani inawezekana,"amesema Mbia

Katibu wa Evawc Piter Amani amesema kwa sasa group hilo lina  wajumbe 26 na  lengo la group hilo ni kuelimisha jamii na kushughulikia watu ambao wameshafanyiwa ukatili wa kijinsia  na kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Aidha Veronica Masawe kutoka Shirika la Women young Leadership (WYL) akishirikiana na Estomine Henry kutoka ofisi ya waandishi wa habari Shinyanga Press Clabu  katika kitengo chao wamefungua Instagram yenye logo ya EVAWC hivyo watu wote  wanawakaribisha
 kufungua na kushea kwa watu mbalimbali ili waweze kusoma kilichomo lengo ni kutokomeza ukatili.

"Pia tuko mbioni kufungua facebook, twitter pamoja na you tubu ili kuhakikisha tunawifikia watu wote na  ukatili wakijinsia tunautokomeza kabisa usiendelee kuwepo,"amesema Veronika Masawe.

Mwenyekiti wa Shinyanga Ending Violence Against Working Group  Shinyanga (EVAWC  WG) Jonathan  Manyama akizungumza kwenye kikao cha robo mwaka kilichofanyika mjini Shinyanga

Wajumbe wa Shinyanga Ending Violence Against Working Group  Shinyanga (EVAWC  WG) wakiwa kwenye kikao 

Katibu wa Shinyanga Ending Violence Against Working Group  Shinyanga (EVAWC  WG) akizungumza kwenye kikao hicho

Mjumbe wa Shinyanga Ending Violence Against Working Group  Shinyanga (EVAWC  WG) akiwasilisha kazi za group hilo

Mjumbe akichangia jambo kwenye kikao hicho

John Shija  kutoka Shirika la Paceshi akichangia jambo kwenye kikao hicho
Pendo Sawa kutoka wanawake laki moja akiwa kwenye kikao hicho 
Wajumbe wakimsikiliza mwenyekiti akizungumza

Wajumbe wakimsikiliza mwenyekiti akizungumza
Kazi ikiendelea 


Adelina Apolinary kutoka shirika la TRCS 



Mwenyekiti na wajumbe wake wakimsikiliza mjumbe akiwasilisha mpango kazi wa group hilo

Post a Comment

0 Comments