Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Suzy Luhende, Shinyanga Blog
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amewataka wenyeviti wa vitongoji na vijiji kufanya mikutano kwa ajili ya kuwajua walengwa wa Tasaf ili waweze kupata haki yao iliyotolewa na Rais Samia Suluhu.
Licha ya kuwataka wenyeviti hao pia amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita, kufuatilia na kuhakikisha watu waliolalamika hawajaingizwa kwenye Tasaf na wale ambao majina yao yameshaandikwa lakini hawaitwi ili waweze kupatiwa haki yao kwa sababu nao ni watanzania.
Mlolwa ametoa maagizo hayo jana kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM, yaliyofanyika kimkoa katika kata ya Idahina halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, baada ya baadhi ya watu wakiwemo wenye ulemavu kutoa malalamiko yao mbele yake na kudai kuwa hawakuandikishwa kwenye mfuko wa Tasaf na wengine waliandikwa lakini hawasomwi majina yao.
Watu hao waliotoa malalamiko yao ni Nestory Ngunya mkazi wa kata ya Idahina ambaye ni mwenye ulemavu wa viungo aliyelalamika kuwa hajaandikwa jina lake, na bibi Mhoja Dotto ambaye amesema jina lake liliandikwa lakini haitwi.
"Nawaagiza wenyeviti wote wa vitongoji na vijiji mkafanye mikutano ili kuwabaini watu hawa wenye uhitaji nao waweze kupata kile kilichotolewa na Rais waweze kupata kwa sababu ni watanzania na wanastahili kupata, pia mkuu wa wilaya fuatilia suala la watu waliolalamika wawezekuandikwa na wengine wasomwe majina yao,"amesema Mlolwa.
"Tunapoadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM ni pamoja na kutetea wanyonge, hivyo naomba hili mlifanyie kazi haraka inawezekana fedha zake zipo zinakuwa za ujanja unanja tu na wengine, hivyo wewe na mtendaji fuatilieni inawezekana kuna wengine msiwafiche mkakaa kimya," amesisitiza Mlolwa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita amesema ataenda kulifuatilia suala hilo na kuhakikisha hawa watu wanawekwa kwenye mfumo wa Tasaf, lakini pia kuna fedha kwa ajili ya wanawake asilimia nne, vijana asilimia nne na watu wenye ulemavu asilimia mbili ataenda kufuatilia ili Nestory Ngunya mwenye ulemavu aweze kupatiwa.
Katika maadhimisho hayo walihudhulia viongozi mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi ambaye alisisitiza wazazi waweze kuwapa malezi mema na kuwafundisha maadili mema watoto ili kwa baadae waweze kuwa na vijana wanaojitambua ambao watalitumikia Taifa na kuleta maendeleo.
Katika maadhimisho hayo jumla ya wanachama 500 walipewa kadi za chama cha mapinduzi kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Shinyanga wengine walihama kutoka vyama vingine vya siasa na kuhamia CCM hivyo Mabala alisema zoezi hilo linaendelea watu wote wa mkoa wa Shinyanga wanakaribishwa kujiunga na CCM.
Naye mbunge wa jimbo hilo Emmanuel Cherehani alimshukuru Rais Samia Suluhu kwa kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi akizungumza kwenye maadhimisho ya mika 46 ya kuzaliwa kwa CCM
Katibu wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu kulia ni katibu wa vijana CCM Mkoa na viongozi wengine wa CCM mkoa wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM
Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akipokea cheti cha pongezi alichoandaliwa na viongozi wa CCM Mkoa
Bibi Mhoja Dotto akitoa malalamiko yake ya kutoitwa kwenye Tasaf kwenye maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM
Nestory Ngunya ambaye ni mwenye ulemavu wa viungo baada ya kutoa malalamiko yake kwa mwenyekiti
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Idahina akizungumza
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa Mabala Mlolwa akitoa cheti cha pongezi kwa mwanachama
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kizaliwa kwa CCM
Viongozi wa CCM Mkoa wakiapa baada ya kigawa kadi za CCM
Kazi ikiendelea katika maadhimisho ya CCM
Kazi ikiendelea kwa vijana wa hamasa na viongozi wake akiwepo katibu muenezi wa Ngokolo na Ndembezi wakiwa wameweka dole kwa furaha ya maadhimisho hayo
Wenyeviti wa jumuia ya wazazi na viongozi mbalimbali wa CCM
Mjumbe wa baraza la wanawake UWT mkoa wa Shinyanga akiwa na viongozi mbalimbali
Viongozi wa CCM wakiwa kwenye maadhimisha ya Chama hicho
Madiwani wa viti maalumu na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga
Kazi ikiendelea
Mwananchi akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo
Kazi ikiendelea katika maadhimisho hayo
Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akiahidi kumhudumia Nestory Ngunya ili aweze kuandikwa Tasaf.
0 Comments