Header Ads Widget

NYAMA CHANZO CHA MWANAFUNZI WA SEKONDARI KUPATA UJAUZITO


Muuza nyama (buchani) Samwel Yohana Lindi mjini anatuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari mwenye umri wa miaka 16 kwa kumhonga nyama.
Pamoja na serikali kufanya juhudi za kukabiliana na tatizo la wanafunzi wa kike kukatisha masomo kwa ajili ya mimba lakini hali bado sio nzuri kwa shule za sekondari mkoani Lindi.


Muuza nyama huyo inadaiwa amemshawishi mwanafunzi huyo kumpa nyama na kumsababishia kupata ujauzito uliomfanya ashindwe kuendelea na masomo bada ya uongozi wa shule kumsimamisha kwa mujibu wa sheria za shule


Mkuu wa Shule ya Sekondari Lindi, Ramadhani Dibelle amekiri kuwepo kwa matukio ya wanafunzi kupata mimba shuleni hapo.


"Tatizo hili lipo katika shule yangu kwani mwaka 2022/wanafunzi wawili, Amina Mpwawa na Nasra Hasani wamepata mimba, mmoja kajifungua amerudi darasani na kufanikiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne na amepata daraja pili," amesema Divelle.
 
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments