Header Ads Widget

UHAMIAJI SHINYANGA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI WIKI YA SHERIA KUELEZEA HUDUMA MBALIMBALI ZA JESHI HILO

Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na Jeshi la Uhamiaji wakati wa uzinduzi wa wiki ya Sheria mkoani wa Shinyanga.

Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga limeshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa elimu juu ya huduma wanazotoa ikiwemo Utoaji Pasipoti, Vibali vya Ukaazi, Vibali vya kuingia nchini (Visa),kudhibiti uhamiaji haramu, kuendesha kesi za uhamiaji haramu pamoja na kupokea maombi ya uraia.

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Mkoani Shinyanga yamezinduliwa rasmi leo Januari 22, 2023 katika Uwanja wa Zimamoto uliopo Manispaa ya Shinyanga.

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka 2023 iliyoanza leo nchini na kutarajiwa kuhitimishwa Februari 1,2023 yanayoongozwa na kauli inayosema, “Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu wajibu wa mahakama na wadau”.

Akizungumza wakati Mgeni Rasmi alipotembelea banda la uhamiaji kwenye  Maadhimisho hayo, Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike amesema wanatumia fursa ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kutoa elimu kwa jamii kuhusu huduma zinazotolewa Uhamiaji ambazo ni pamoja na kukagua Fomu za maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) sambamba na huduma ya uendeshaji wa kesi zinazohusu wahamiaji haramu na kupokea maombi ya uraia wa Tanzania.

Angumbwike amezitaja huduma zingine wanazotoa kuwa ni Utoaji wa Hati ya Kusafiria (Pasipoti), huduma ya vibali vya ukaazi, vibali vya kuingia nchini (Visa) na huduma ya kudhibiti wahamiaji haramu.

Angumbwike amesema pia Uhamiaji inatoa Huduma kwa njia ya Mtandao hivyo kuwahamasisha wananchi kutumia fursa ya Mtandao kupata huduma zinazotolewa Uhamiaji.

" kwa njia ya mtandao ni huduma mpya inayomuwezesha muombaji kujaza Fomu ya Maombi ya Pasipoti kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote. Baada ya kujaza fomu hiyo, atatakiwa kuichapisha (Print) na kuiwasilisha pamoja na vielelezo vingine katika Ofisi ya Uhamiaji iliyo karibu naye kwa ajili ya kushughulikiwa maombi yake ya Pasipoti",amesema Angumbwike.

Akizungumza wakati akifungua maadhimisho hayo, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga watumie fursa ya maadhimisho hayo ya wiki ya Sheria kupata elimu na msaada wa kisheria bure na kupata ufumbuzi wa matatizo yao.
 
Naye Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma, alikazia pia suala la utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi, na kueleza kuwa ni njia ambayo itapunguza pia mrundikano wa kesi mahakamani

Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na Jeshi la Uhamiaji wakati wa uzinduzi wa wiki ya Sheria mkoani Shinyanga.
Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na Jeshi la Uhamiaji wakati wa uzinduzi wa wiki ya Sheria mkoani Shinyanga.
Uzinduzi wiki ya sheria mkoani Shinyanga ukiendelea.

Uzinduzi wiki ya sheria mkoani Shinyanga ukiendelea.

Uzinduzi wiki ya sheria mkoani Shinyanga ukiendelea.

Maafisa mbalimbali wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria mkoani Shinyanga.
Maafisa Uhamiaji wakipiga picha ya pamoja na viongozi kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Shinyanga.
Maandamano yakiendelea kwenye uzinduzi wa wiki ya sheria mkoani Shinyanga.
Maandamano yakiendelea kwenye uzinduzi wa wiki ya sheria mkoani Shinyanga.
Maandamano yakiendelea kwenye uzinduzi wa wiki ya sheria mkoani Shinyanga.
Maandamano yakiendelea kwenye uzinduzi wa wiki ya sheria mkoani Shinyanga.Maandamano yakiendelea kwenye uzinduzi wa wiki ya sheria mkoani Shinyanga.
 
PICHA; NA MARCO MADUHU.

Post a Comment

0 Comments