Header Ads Widget

WANASHERIA, WAENDESHA MASHTAKA NA WAPELELEZI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAPATIWA MAFUNZO JIJINI MWANZA


Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Lucy E Saleko akizungumza kabla ya kuanza kwa Mafunzo kwa Wanasheria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Mwanza.
Baadhi ya Wanasheria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Mahakimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Maliasili na Utali, Lucy E, Salekoi kwenye Mafunzo ya Wataalamu hao yanayofanyika Jijini Mwanza.


Na John Bera - Mwanza

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Kitengo cha Huduma za Sheria imeendesha mafunzo kwa Wanasheria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya Wizara hiyo ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria za kisekta na Sheria Mtambuka kwa lengo la kupunguza matukio ya ujangili wa mazao ya misitu na wanyamapori kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Lucy Saleko  amesema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa na Kitengo cha Sheria chini ya udhamini wa Mradi wa Kuzuia na Kupambana na ujangili wa wanyamapori na Biashara haramu ya nyara na mazao ya misitu (CPIWT Project), UNDP na Global Environmental Facility (GEF) chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.


“Sisi kama kitengo cha Sheria ambao ndio waratibu wakuu wa mafunzo haya tumekuwa tukipata changamoto hususan kwenye makosa ya ujangili na mifugo kukamatwa kutokana na watu kuingiza hifadhini, mafunzo haya ni muhimu pale mashauri yanapopelekwa mahakamani kuhakikisha ushahidi unatolewa wa mtu aliyeingiza mifugo hifadhini haukwami", amesisitiza Lucy Saleko.


Amesema kutokana mafunzo hayo,Washeria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wataongeza ujuzi katika kudhibitisha vielelezo vya ushahidi na kukusanya taarifa za ushahidi wawapo mahakamani.

Post a Comment

0 Comments