Header Ads Widget

JAMII YA LYABUKANDE YABAINISHA MAENEO HATARISHI KWA WATOTO DHIDI YA UKATILI NA IMEKUBALI KUCHANGIA CHAKULA MASHULENI.

JAMII YA LYABUKANDE YABAINISHA MAENEO HATARISHI KWA WATOTO DHIDI YA UKATILI NA IMEKUBALI KUCHANGIA CHAKULA MASHULENI.

Mwakilishi wa wanawake kata ya Lyabukande akiwasilisha hoja zake.

Mkurugenzi wa shirika la WEADO akielezea utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili.

Mratibu wa Dawati la Jinsia Mkoa, Afande Monica Sehere ametoa wito kwa wanajamii kushirikiana na vyombo vya dola katika utoaji wa taarifa za vitendo

Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Lyabukande, Salum Mwang'mba akitoa taarifa ya matukio ya ukati katika kata ya Lyabukande.

Na Mwandishi wetu.

Shirika la Women Elderly Advocacy and Development Organization (WEADO) limeongoza zoezi la kutambulisha mradi wa "Chukua Hatua Sasa: Zuia Ukatili" na kupanga mkakati wa kukabiliana na vitendo vyote vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Kata ya Lyabukande, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. 

Utambulisho wa mradi umefanywa Novemba,2022 katika kata ya Lyabukande na Mkurugenzi wa WEADO  Elyasenya Nnko.Shirika la WEADO litatekeleza mradi huo  kwa kipindi cha miezi mitatu (Novemba 2022 hadi Januari 2022 kwa ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania.

Shughuli hiyo kutambulisha mradi huo ,iliwakutanisha Viongozi wa mamlaka ya Serikali za Mitaa,  Diwani, wenyeviti wa vijiji, Watendaji wa vijijj, wawakilishi wa vikundi vya wanawake, wawakilishi wa Baraza la watoto Kata, Viongozi wa dini, Mratibu wa Dawati la Jinsia mkoa, Afisa Maendeleo ya Jamii, Wazee wa kimila na Mratibu Elimu Kata kutoka kata Lyabukande.

Elyasenya alisema,Kusudio letu katika huu ni kuunganisha nguvu na kuwa na ushawishi kwa kila moja wetu ili tuweze kuwa na mazingira salama kwa wanawake na watoto.

"Mradi huu unatambulishwa kwenu ili kupata ridhaa yenu, ushirikiano wenu na tuweke mikakati ya pamoja ya kutengeneza mazingira salama yasiyo na ukatili kwa wanawake na watoto" Alisema Elyasenya

Naye Afisa Mradi kutoka WEADO, John Eddy amesema kwamba Mradi huu umekuja wakati mwafaka ambapo Serikali na wadau wanaungana kuhamasisha Jamii kuchukua hatua madhuhutii ya kukomesha Ukatili.

"Tumefanya semina nyingi sana, tumekuwa na vikao vingi sana Kama hivi, imetosha sasa, kilichobaki ni kuchukua hatua za kufichua matendo ya ukatili na kutoa taarifa na kushiriki katika mchakato wa kutoa  ushahidi" Alisema Afisa Mradi huyo.

Kwa upande wao, wenyeviti, Watendaji wa vijiji na wawakilishi wa Jamii walibainisha maeneo hatarishi katika vijiji/ Vitongoji ambapo watoto wanakumbana na vitendo vya ukatili. Maeneo hayo ni vilabu vya pombe, sehemu za michezo ya bahati nasibu, sherehe za usiku na ngoma, gulioni, maeneo ya center na nyumba za kulala wageni.

Akielezea mikakati iliyopo, Mh. Diwani wa Kata ya Lyabukande, Luhende Kawiza amesema kata ya Lyabukande imeweka makazo mahususi kwa wanajamii wote kutoruhusu watoto na wasichana kufika maeneo hayo bila utaratibu wa uangalizi unaozingatia ulinzi na usalama wa mtoto. 
Wakichangia katika kikao hicho, wanajamii wamekubaliana kuwasaidia watoto kupata chakula cha mchana shuleni ili kuwaepusha na vishawishi vya kujihusisha na mahusiano ya kingono na kuepuka ukatili wa kingono.

Naye,Mratibu wa Dawati la Jinsia Mkoa, Afande Monica Sehere ametoa wito kwa wanajamii kushirikiana na vyombo vya dola katika utoaji wa taarifa za vitendo vyote vya ukatili na kushiriki katika mchakato wa ushahidi.

 Aidha,akitoa taarifa ya hali ya ukatili katika Kata ya Lyabukande, Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Lyabukande, Salum Mwang'mba   alisema kwamba katika kipindi  cha mwaka 2021/2022 jumla ya matukio 11 yaliripotiwa katika Ofisi ya Kata ambapo matukio ya Ukatili wa mwili ni 3, ukatili wa kingono 2, matukio ya utelekezaji 2, matukio ya unyanyasaji 2 na unyang'anyi 2. Katika matukio hayo 11, mawili yalithibitishwa kutokuwa na ukweli wowote, matukio 4 yalikatiwa rufaa polisi na mengine yalipatiwa suluhu kupitia kamati ya MTAKUWWA ya kata.
 
"Jamii imeanza kuhamasika katika utoaji wa taarifa ya matukio ya Ukatili. Hata hivyo jamii inaogopa kutoa ushahidi mahakamani wakati  wa kuendesha mashauri" Alisema Afisa Maendeleo ya Jamii. 

Kwa upande wake Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndugu Edmund Adon ametoa wito kwa washiriki kwenda kuwa mabalozi kwa Jamii nzima.

Post a Comment

0 Comments