Header Ads Widget

ASKOFU SANGU AKEMEA KUSHEREHEKEA SIKUKUU KWA MATENDO YA GIZA, ATAMANI MVUA INYESHE KUTWA NZIMA


ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akiongoza Ibada kwenye mkesha wa Sikukuu ya Christmas.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, akiwa kwenye Ibada ya mkesha wa Sikukuu ya Christmas

Muonekano wa baadhi ya Waumini wa Kanisa Katoliki Shinyanga Mjini wakiwa kwenye mkesha wa Sikukuu ya Christmas.

Wanakwaya wa Kanisa Katoliki Shinyanga Mjini wakiwa kwenye mkesha wa Sikukuu ya Christmas.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, amewataka watanzania washerehekee siku kuu ya Christmasi (Noeli) wakiwa nyumbani na watoto wao, pamoja na kusaidia watu wenye uhitaji na siyo kuitumia siku hiyo kwa kutenda matendo ya giza.

Askofu Sangu amebainisha hayo jana kwenye Mkesha wa Sikukuu ya Christimas, Ibada iliyofanyika Kanisa Katoliki Shinyanga Mjini la Moyo safi wa Maria.

Amesema Sikukuu ya Christimas ni sherehe ya kuzaliwa mkombozi Yesu Kristo, hivyo ni vyema watu wakaisherehekea kwa upendo, amani na kusaidia watu wenye uhitaji, na siyo kutenda matendo ya giza ikiwamo ulevi.

“Nawaombeni watanzania tusherehekee sikukuu hii ya Christmas majumbani tukiwa na watoto wetu au kwenda kusaidia watu wenye uhitaji, na siyo kuitumia kwa kutenda mambo ya giza, na wakati mwingine hua natamani mvua inyesha kuanzia asubuhi hadi saa sita usiku ili watu wasitoke wabaki na familia zao,”amesema Askofu Sangu.

Katika hatua nyingine Askofu Sangu, amewataka wananchi wawe na Kristo ndani ya mioyo yao pamoja na hofu ya Mungu, ili kudumisha amani hapa duniani sababu imeonekana kupungua kutokana na kuendelea kwa matukio mabaya ikiwamo Vita, Mauaji, na ukatili dhidi ya watoto wadogo.

“Dunia imepungukiwa na amani sababu watu hawana Kristo mioyoni mwao wala hofu ya mungu, ndiyo maana kila kukicha tunashuhudia matukio ya ajabu, watu wanauwana hovyo”amesema Askofu Sangu.

Aidha, amesema Chibuko la Amani pekee ni kumpokea Yesu Kristo ndani ya mioyo, na hakutakuwa tena na machafuko, mafarakano, ugomvi, ufisadi,vita, mauaji ya watu wasio na hatia, wala vitendo vya ukatili.

Pia Askofu Sangu, amelipongeza Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kwa kupiga marufuku Disco Toto, pamoja na kudumisha Amani kwenye nyumba za Ibada katika mikesha ya Sikukuu.

Muonekano wa baadhi ya Waumini wa Kanisa Katoliki Shinyanga Mjini wakiwa kwenye mkesha wa Sikukuu ya Christmas.

Post a Comment

0 Comments