Header Ads Widget

FAMILY DAY YA MGODI WA NORTH MARA YAKUTANISHA FAMILIA ZA WAFANYAKAZI NA JAMII INAYOISHI NA MGODI KUFURAHI PAMOJA


Michezo ya watoto ikiendelea
Mgodi wa dhahabu wa North Mara mwishoni mwa wiki uliandaa tukio la family Day 2022, ambalo lilikutanisha maelfu ya wanafamilia wa wafanyakazi wa Mgodi huo ,viongozi wa Serikali na vijiji vinavyozunguka mgodi, na wakazi wa eneo hilo ambapo waliweza kuungana na kufurahi pamoja kuadhimisha siku hiyo.

Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya ‘Kazi na Familia’ yalipambwa na maonesho ya shughuli zinazofanyika katika mgodi huo, michezo mbalimbali ya watu wakubwa na watoto, chakula cha pamoja, vinywaji , muziki na kubadilishana mawazo.


Mgodi wa North Mara upo eneo la Nyamongo katika wilaya ya Tarime mkoani Mara, ukiendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.

Katika hotuba yake katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele imeeleza kufurahishwa na namna mgodi huo unavyojali familia za wafanyakazi wake kiasi cha kuwaalika kwenda kuona wanavyofanya kazi.

“Tumeendelea kuwa na ushirikiano mzuri na Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara. Kwa niaba ya Serikali niwaahidi tutaendelea kushirikiana nanyi katika kuhakikisha mnafikia dhamira yenu katika viwango vya juu zaidi,” alisema.


Amesema kuwa ni matumaini yake kwamba Barrick North Mara itaweza kufikia malengo yake kwa kuendelea kuyapa kipaumbele maadili ya msingi ya kuwa na usalama mahala pa kazi wakati wote,

“Uwajibikaji na uadilifu, matokeo chanya, ubia, kuwa na watu wa kiwango cha kimataifa, ukweli, uwazi na uadilifu yatafanya mfikie dhamira yenu,” imesema sehemu ya hotuba ya Mkuu huyo wa Wilaya.


Akaongeza kuwa kauli mbiu ya Siku ya Familia ya Barrick North Mara 2022 inayosema “Kazi na Familia” inaakisi dhamira ya Serikali ya kutaka watu wafanye kazi kwa kujituma huku wakikumbuka malezi bora kwa familia zao.

“Nimefarijika kuwaona hapa viongozi wa vijiji vinavyozunguka eneo la mgodi. Sisi kama Serikali kupitia mkusanyiko huu tunahamasisha mshikamano, ujirani mwema, amani na upendo kati ya mgodi na vijiji vinavyouzunguka.


“Mshikamano huu utazidi kujenga urafiki na hivyo kuleta faida kwa pande zote, yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwekezaji wetu Barrick na wananchi wanaozunguka mgodi,” imeongeza sehemu ya hotuba ya Kanali Mntenjele.

Kwa upande wake Meneja wa Mkuu wa Mgodi huo ,Apolinary Lyambiko aliwakakaribisha na kuwashukuru wote waliohudhuria hafla hiyo ambayo imewezesha wanafamilia za wafanyakazi kuona kazi zinazofanywa na mgodi sambamba na kudumisha mshikamano na jamii inayozunguka mgodi huo.

Nao baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo walipongeza mgodi huo kwa kuandaa siku hiyo kubwa ambayo mbali na kujumuisha wafanyakazi na familia zao pia inawaunganisha na viongozi wa vijiji jirani na wananchi wanaoishi katika eneo hilo.
Mbunge wa Tarime Vijijini,Mwita Waitara (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kuhusu kifaa cha uokozi kinavyofanya kazi kutoka kwa mfanyakazi wa Mgodi wa North Mara wakati wa maonyesho ya Family Day 2022, wa kwanza kulia ni Meneja wa Mgodi huo,Apolinary Lyambiko.
Michezo ya watoto ikiendelea
Mchezo wa kufukuza kuku ukiendelea
Michezo ikiendelea
Michezo ikiendelea

Post a Comment

0 Comments