Header Ads Widget

RC SHINYANGA AUPONGEZA UONGOZI WA KAMPUNI YA MGODI WA ALMAS WLD MWADUI KWA KUSAINI MKATABA WA KUBORESHA MASIRAHI YA WAFANYAKAZI



Meneja wa mgodi wa Willamson Mhandisi Ayubu Mwenda akiwa na katibu mkuu Tamico Patenus Rwechungula wakionyesha wa wafanyakazi waliosaini 

Suzy Luhende, Shinyanga blog

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema ameupongeza uongozi wa mgodi wa madini ya almasi Mwadui Williamson Diamod (WLD) ulioko  katika wilaya ya  Kishapu mkoani Shinyanga kwa kusaini mkataba wa hali  bora ya wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kuboresha masirahi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, 

Pongezi hizo amezitoa leo wakati akishuhudia utiaji saini mkataba wa hali bora ya wafanyakazi wa kampuni hiyo  uliofungwa baina ya mgodi huo na Chama cha wafanyakazi wa migodini Tamico uliofanyika katika viwanja vya Mwadui ambapo ameipongeza  kampuni hiyo kwa kuwathamini wafanyakazi  na kuweza kuwaboreshea masirahi yao.

Mjema amesema kwa hicho kilichofanyika leo anaitaka na migodi mingine, taasisi mbalimbali ziboreshe masrahi ya wafanyakazi wake ili waweze kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi zaidi na kwa kutimiza matakwa ya wafanyakazi.

,"Bila wafanyakazi kuboreshewa masirahi yao hali ya kufanya kazi inakuwa ni ya kusua sua, lakini  akiboreshewa anakuwa na mori ya kuweza kufanya kazi, hivyo tunakushukuru sana meneja  wa mgodi huu kwa sababu unamuunga mkono Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu, hivyo na taasisi zote zihakikishe zinawa mikataba wafanyakazi wake,"amesema Mjema.

,"Hakikisheni mnafanya kazi kwa weledi mkubwa na kupendana kwa sababu mmeboreshewa masilahi yenu, pia mhakikishe,  mnasainiwa na kamishina  wa kazi ili uanze kufanya kazi mara moja, kwani mkataba huu una lengo la kukuza fursa na kuboresha utendaji wa kazi,"amesisitiza Mjema.

Aidha Mjema  amewataka wahakikishe wageni wote wanaofika katika kampuni wanakuwa na vibali maalumu vya kufanya kazi kwa kanuni na sheria ya nchi,"amesema mkuu wa mkoa Mjema.

Kwa upande wake meneja mkuu wa mgodi wa WLD mhandisi Ayubu Mwenda amesema ni muda mrefu hawakuwa na mkataba wa namna hiyo kwa sababu ya ugonjwa wa Covid 19, lakini kwa vile alikuwa na malengo ya kuboresha maisha ya wafanyakazi pamoja na kuboresha mahusiano na majirani pamoja na serikali amelitimiza lengo hilo.

"Baada ya kuingia hapa tulikubaliana na wafanyakazi kuwa tutaboresha masirahi ya wafanyakazi, na pia tusisahau kwamba shughuli za uzalishaji zikiongezeka ndio itatuwezesha kuwa na mchango kwenye uchumi wa nchi, mkoa, wilaya na kwenye vijiji vinavyotuzunguka michango itaongezeka zaidi,"amesema.

Naye katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa migodi TAMICO Patenus Rwechungula amesema kupitia mkataba wa hali bora tutaenda kuboresha zaidi wanaamini baada ya miaka mitatu mkataba huo utaendelea, hivyo wafanyakazi waliokengeuka wakaenda kusikojulikana  warudi kwenye vyama vya wafanyakazi.

,"Sisi tunaamini mkataba huu utaleta ufanisi zaidi kwa wafanyakazi na hamasa kubwa, hivyo tutaweza kumshawishi mwajili tuendelee katika kiwango cha juu, hivyo wafanyakazi waliokengeuka rudini kwenye shina, hivyo leo tamico inashukuru kwa tukio hili tunaheshimu majadiliano, kwani mkataba huu utadumu kwa muda wa miaka mitatu,"amesema Rwechungula

Akisoma risala katibu tawi Gatti Raphael amesema anaishukuru kampuni hiyo kwakuthamini wafanyakazi wake, kwani hata baada ya kutokea ugonjwa wa Covid 19 haikupoteza hata mfanyakazi mmoja wameshukuru kwa kuwapatia mkataba hivyo wamesema watafanya kazi kwa weledi na kwa bidii kwa sababu wameboreshewa masirahi yao.



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga   Sophia Mjema akionyesha keki iliyoandaliwa na wafanyakazi wa mgodi huo 


Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akilishwa keki na mfanyakazi wa mgodi huo



Mfanyakazi wa mgodi wa WLD akiandaa keki iliyoandaliwa na wafanyakazi


Mkuu wa mkoa na viongozi wenzake wakiibariki keki kabla ya kukata



Meneja wa mgodi wa WLD akiwa na katibu mkuu wa Tamico wakisaini mkataba wa wafanyakazi

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza 


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia  Mjema akishuhudia wakisaini mkataba wa wafanyakazi wa mgodi wa kampuni ya WLD 



Mfanyakazi akimlisha keki meneja wa mgodi wa WLD

Meneja wa mgodi wa WLD  na katibu mkuu wa TAMICO wakionyesha mikataba hiyo baada ya kusaini




Meneja wa mgodi wa WDL mhandisi Ayubu Mwenda akizungumza 



Katibu mkuu wa Tamico Patenus Rwechungula akizungumza na kuushukuru uongozi wa mgodi kwa kuboresha masirahi ya wafanyakazi


Wafanyakazi wa mgodi wa WLD wakiwa kwenye tukio la utiaji saini mkataba wa wafanyakazi


Wafanyakazi wa mgodi wa WLD wakiwa kwenye tukio la utiaji saini mkataba wa wafanyakazi

Wageni waalikwa na viongozi wa dini wakiwa katika tukio la utiaji saini mkataba wa wafanyakazi

Post a Comment

0 Comments