Header Ads Widget

MKEMIA MKUU WA SERIKALI ATOA TAARIFA KUWA MAJI YA BWAWA LA MAJITOPE YA MGODI WA ALMASI WA WILLIAMSON DIAMOND (WDL) HAYANA MADHARA KWA BINADAMU NA KWA WANYAMA


Meneja ofisi ya mkemia mkuu wa serikali  kanda ya ziwa Mwanza Musa Kuzumila akitoa taarifa za majitope ya bwawa la mgodi wa almasi wa WDL

Suzy Luhende, Shinyanga Blog

Meneja ofisi ya mkemia mkuu wa serikali  kanda ya ziwa Mwanza Musa Kuzumila amesema wamefanya upimaji wa maji na tope ya bwawa lililopasuka  la mgodi wa almasi wa Williamson Diamond Ltd (WDL) na kukuta kwamba maji hayo hayana madhara kwa binadamu na wanyama, hivyo wananchi wanaruhusiwa kutumia na kunywesha mifugo kama kawaida.

Hayo ameyasema leo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo amesema wamefanya upimaji wa maji na tope na kuonekana hayana madhara ya aina yeyote, hivyo wananchi waondoe hofu waendelee kutumia maji hayo.

 "Tulianza upimaji wa sampuli tarehe 9mwezi huu baada ya tukio hili kutokea tulipima maji na tope ambapo tulichukua maji magarbi mwa bwawa la almas na upande wa kwenye vijiji vilivyoathirika, hivyo tulibaini tope na maji hayana kemikali ya aina yoyote, maji hayo yapo salama hivyo tunawaomba wananchi wasiwe na hofu tena,"amesema Kuzumila.

Kwa upande wake meneja NEMC kanda ya ziwa mwanza Jarome Kayombo alisema  kuna uchunguzi mbalimbali umefanyika kuhusiana na bwawa hilo kupasuka ofisi ya mkemia wamepima wameona maji hayo  hayana madhara kwa wananchi na kwa wanyama.

Naye mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema alisema baada ya bwawa kupasuka maji kutiririka wananchi walishindwa kutumia maji kwa kuhofia yana madhara, lakini vipimo vimeonyesha maji haya ni salama, hivyo wanatakiwa kutumia bila wasiwasi.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu  Joseph  Mkude alisema taharuki kwa wananchi wa Wilaya ya Kishapu ilikuwa kubwa lakini kwa sasa wataalamu wametangaza maji hayo hayana madhara waendelee kutumia na kunywesha mifugo.

" Tume tuliipa siku saba kwa ajili ya uchunguzi kwa ajili ya unyeti  wa utaalamu na taarifa ya awali sasa wananchi wasiwe na hofu tena maji hayo yamepimwa hayana madhara, hivyo kuna uhakika hivyo waendelee kutumia tu  bila hofu, na tume tumeiongezea muda wa kufanya uchunguzi zaidi mpaka tarehe 20 mwezi huu,"alisema Mjema.

"Baada ya bwawa la majitope kubomoka taharuki ilikuwa kubwa, kwamba maji hayo siyo salama lakini leo nafarijika kudikia kwamba maji hayo hayana madhara, nashukuru kwa kutangaziwa na mkuu wa mkoa pamoja na mkemia mkuu wa serikali, hivyo wananchi wangu wasiwe na wasi wasi tena maji ni salama kabisa,"alisema Mkude.

Viongozi mbalimbali wakisikiliza taarifa ya mkemia mkuu 


Meneja ofisi ya mkemia mkuu wa serikali  kanda ya ziwa Mwanza Musa Kuzumila akitoa taarifa za majitope ya bwawa la mgodi wa almasi wa WDL

Kwa upande wake meneja NEMC kanda ya ziwa mwanza Jarome Kayombo 

 Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza



Viongozi mbalimbali wakisikiliza taarifa ya mkemia mkuu wa serikali akitoa taarifa




Post a Comment

0 Comments