Header Ads Widget

MABALA MLOLWA ATETEA KITI CHAKE CHA MWENYEKITI CCM MKOA WA SHINYANGA, GAKI ASHINDA UNEC KWA MBINDE KWA KURA 10

MABALA ASHINDA KWA KISHINDO UENYEKITI CCM MKOA WA SHINYANGA, GAKI APETA UNEC

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa atetea kiti chake kwa mara nyingine tena uchaguzi wa CCM.

 

MNEC Gaspar Kileo (GAKI) MNEC atetea kiti chake kwa mara nyingine tena uchaguzi wa CCM.

Na Mwandishi Wetu 


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Kashindye Mlolwa amefanikiwa kutetea kiti chake kwa kipindi kingine cha miaka mitano akiwashinda washindani wake kwa kura 668 huku Gasper Hanson Kileo (GAKI) naye akifanikiwa kutetea nafasi yake ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM (NEC).Akitangaza matokeo ya uchaguzi leo Jumatatu Novemba 21,2022
kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga, Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Thobias Andengenye amesema Wajumbe walioshiriki katika uchaguzi huo walikuwa 757 kura moja imeharibika na kura halali zilikuwa 756 ambapo Mabala Mlolwa amepata kura 668, huku Costantine Molo Nkuba kura 35 na Eliaza Onael Kanuya kura 53.

Andengenye amemtangaza Mabala Mlowa kuwa mshindi katika nafasi ya uenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga kwa kipindi cha miaka mitano na katika nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC) mshindi Gasper Hason Kileo ambaye pia alikuwa akitetea nafasi yake.

Wagombea katika nafasi ya MNEC, wapiga kura walikuwa 754 kura moja imeharibika na kura halali zilikuwa 753 ambapo Gasper Hanson Kileo amepata kura 380, Dkt. Majuto Clement Manyilizu kura 370 na Nyasiro Maiga Magogo kura tatu.

Andengenye ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amewashukuru wajumbe kwa ushirikiano na demokrasia waliyoionesha katika uchanguzi huo ambao umefanyika kwa uhuru na haki.

Akitoa neno la shukrani kwa wajumbe waliomchagua kuwa mwenyekiti Mabala amesema wajumbe wamempa deni kubwa na hivyo ameahidi kushirikiana na viongozi wenzake kukijenga Chama Cha Mapinduzi hali itakayosaidia kuchochea maendeleo ya chama hicho.

"Mimi kwa kushirikiana na viongozi wenzangu tutafanya kazi ya kuchochea maendeleo ya Chama Cha Mapinduzi ikiwa ni pamoja na kuyatangaza mazuri yote yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kukijenga chama na kuchochea maendeleo ya wananchi”, amesema Mabala.

Naye Gaspar Kileo amewashukuru wajumbe baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika nafasi hiyo ameahidi kuwa mwaminifu wakati wa kukitumikia chama h hicho huku akiwashukuru wajumbe kutoka katika halmashauri zote za mkoa wa Shinyanga kwa kumpa nafasi ya kuongoza tena chama hicho katika nafasi ya mjumbe wa halimashauri Kuu Taifa (MNEC).

“Niwapongeze wajumbe wote kutoka katika halimashauri zote za mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kuniamini tena na kunipa nafasi hii”, amesema Kileo.

Nao baadhi ya wajumbe walio shirikikatika uchaguzi huo akiwemo mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanel Cherehani ameeleza kuwa wameridhishwa na usimamizi wa uchaguzi huo kwa sababu wanaamini viongozi waliochaguliwa watakisimamia na kukiongoza chama katika kipindi cha miaka 5.

Msimamizi mkuu wa uchaguzi , Thobias Andengenye akizungumza wakati wa mkutano wa uchaguzi

Post a Comment

0 Comments