Header Ads Widget

SHINYANGA KUTOA CHANJO YA POLIO KWA WATOTO 521,025

Mratibu wa Chanjo mkoani Shinyanga Timothy Sosoma akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampeni ya utoaji Chanjo ya Polio awamu ya Nne kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKOA wa Shinyanga unatarajia kutoa chanjo ya matone ya Polio kwa watoto wapatao 521,025, kwa ajili ya kuwakinga na ugonjwa wa kupooza wa Polio.

Mratibu wa Chanjo mkoani Shinyanga Timothy Sosoma, amebainisha hayo leo Novemba 29, 2022 wakati akitoa taarifa ya kampeni ya chanjo hiyo ya matone ya Polio, ambayo itatolewa kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano itakayo anza kutolewa Decemba Mosi mwaka huu hadi tarehe 4.

Amesema Mkoa huo umeshapokea jumla ya dozi ya chanjo ya Polio 614,800 na walengwa wote watafikiwa na timu ya wataalam 1,021.

"Kampeni hii ya chanjo ya matone ya Polio tutaitoa nyumba kwa nyumba, sokoni, stendi za mabasi, lengo ni kufikia idadi ya watoto wote 521,025 ambao tumetarajia kuwapatia chanjo hii,"amesema Sosoma.

Naye Kaimu Maganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu, ameitaka jamii kutoa ushirikiano wa kutosha kwa watoto wao kuwapatia Chanjo hiyo, na kueleza kinga ni bora kuliko Tiba.
Kaimu Maganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu, akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampeni hiyo ya Chanjo ya Matone ya Polio kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.

Mratibu wa Chanjo mkoani Shinyanga Timothy Sosoma akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampeni ya utoaji Chanjo ya Polio awamu ya Nne kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.

Waandishi wa habari wakichukua taarifa juu ya kampeni ya utoaji Chanjo ya Polio kwa njia ya matone dhidi ya watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.

Waandishi wa habari wakichukua taarifa juu ya kampeni ya utoaji Chanjo ya Polio kwa njia ya matone dhidi ya watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.

Post a Comment

0 Comments