
Baadhi ya wafanyabiashara halmahsuari ya Ushetu wakimsikiliza afisa msimamizi wa kodi kanda ya ziwa kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Morgan Isdory.
Na Neema Sawaka, Kahama
MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa kodi Kahama Imewataka wafanyabiashara kutunza kumbukumbu zao za biashara kwa mujibu wa sheria ya fedha ya mwaka 2022 .
 Afisa msimamizi  wa kodi kutoka  kanda
ya ziwa Morgan Isdory  amesema hayo   jana wakati akitoa elimu ya mlipa kodi kwa
wafanyabiashara wa halmashauri ya Ushetu.
Isidory  amesema  wapo pia wafanyabiashara ambao wamekuwa  na mashine za EFD na kutotoa risiti kabisa
kwa mteja  na wengine kutoa bei pungufu
kwenye bidhaa tofauti na uhalisia hilo ni kosa na faini yake ni kifungo cha
miaka mitatu au kulipa sh Millioni tatu.
Isdory
amesema nchi zilizoendelea ukwepaji wa kodi ni kosa la jinai  ndiyo maana hapa Tanzania mara kwa mara
kumekuwepo maboresho ya kanuni na sheria.
Isdory
amesema  kwa mujibu wa sheria ya fedha
ya  mwaka 2022  inaeleza kodi itatozwa  kwenye faida 
kwa mfanyabiashara  awe na
uwezo  wa kutunza kumbukumbu.
“Uzingatiaji  wa 
kifungu  cha 35 cha sheria ya  usimamizi wa kodi na utunzaji wa kumbukumbu
ni muhimu kwa kumfanyabiashara”amesema Isdory.
Isdory
amesema  mfanyabiashara asiye na
kumbukumbu makadirio yanaweza  kuwa
sahihi au  yasiwe sahihi kwake.
Isdory
amesema  kanuni za kodi zinaeleza gharama
ya usafirishaji  haitakiwi kuzidi   kodi anayotakiwa kulipa mfanyabiashara.
Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhulia kupata elimu hiyo Msabaha Issa na Ramadhani Ngau wamesema kodi zimekuwa nyingi kwa mfanyabiashara zingine zipunguzwe ili wapate faida.
Wafanyabiahsra halmahsuari ya Ushetu wakimsikiliza afisa msimamzi wa kodi kanda ya ziwa kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Morgan Isdory.
Wafanyabiahsra halmahsuari ya Ushetu wakimsikiliza afisa msimamzi wa kodi kanda ya ziwa kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Morgan Isdory.

Mfanyabiashara Msabaha Issa akiongea kwenye semina

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464

 
 
       
 
 
