Header Ads Widget

CCM WILAYA YAMPONGEZA MKURUGENZI NA WATUMISHI WOTE KWA KUUBADILISHA MJI WA SHINYANGA NA KUWA WA KISASA

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Magile Anold Makombe akizungumza 

Suzy Luhende Shinyanga Blog

Shinyanga. Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Magile Makombe amempongeza mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura na wataalamu wa manispaa hiyo kwa uthubutu wa kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo, kwani imekuwa ni manispaa ya kuigwa.
Pongezi hizo amezitoa kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa hiyo, ambapo  amesema kutokana na muonekano wa mazingira ya manispaa ya Shinyanga kwa sasa baada ya maboresho wanastahili kupongezwa, ili waweze kuboresha zaidi na zaidi.

Makombe amesema chama cha mapinduzi kinapoona maendeleo yanafanyika kinapata nguvu kubwa ya kukisemea kwa sababu maendeleo yote yanafanyika kupitia ilani ya chama cha mapinduzi CCM, hivyo aliomba juhudi hizo ziendelee ili mji wa Shinyanga uwe na mabadiliko ya kimaendeleo na kuongezeka kwa uchumi.

" Yanapoonekana maendeleo hata kwenye uchaguzi wetu hatutahangaika sana kujieleza kwa maneno kwa sababu maendeleo yanaonekana kwa macho, yanajieleza yenyewe, hivyo nawashukuru sana madiwani Mkurugenzi na watumishi wete kwa ushirikiano wenu, pia namshukuru Rais kwa kutuletea fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo mbalimbali ya wilaya yetu ya Shinyanga mjini,"amesema Makombe.

Aidha katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Ally Majeshi amewapongeza madiwani kwa kuweza kuwasemea wananchi ili waweze kutatuliwa kero mbalimbali zilizopo kwenye kata, hivyo amewataka waendelee kuwasemea na kusimamia miradi mbalimbali iliyopo ili iweze kuwa na ubora unaotakiwa.

"Maendeleo yote yanayofanyika ni kupitia irani ya chama cha mapinduzi CCM, hivyo muendelee kusimamia miradi yote inayotekelezwa kupitia irani yetu,  amesema Majeshi.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa manispaa hiyo Getruda Gisema alishukuru kwa pongezi hizo na kuahidi kuwa watafanya kazi kwa kujituma ili kuhakikisha Shinyanga inakuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo na ya kiuchumi.

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Ally Majeshi akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani baada ya kutembelea 

Afisa utumishi wa manispaa ya Shinyanga Getruda Gisema akishukuru baada ya viongozi wa chama cha mapinduzi CCM kupongeza juhudi za kimaendeleo zinazofanyika mjini hapaPost a Comment

0 Comments