
PROFESA Williamu Mahalu ambaye ni bingwa mbobezi wa upasuaji wa moyo na kifua kutoka Hospitali ya rufaa Bugando.
Na
Kareny  Masasy, Bukombe
PROFESA Williamu Mahalu ambaye ni bingwa mbobezi wa upasuaji wa moyo na kifua kutoka Hospitali ya rufaa Bugando amesema wazazi wengi hawatambui matatizo ya moyo kwa watoto wao.
Na  kati ya watoto laki moja  basi  watoto
15 wanakutwa na magonjwa ya moyo hapa nchini.
Profesa Mahalu
amesema hayo jana  mbele ya waandishi wa
habari  katika hospitali  ya  binafsi
ya Charles Kulwa Memorial iliyopo Ruzewe wilayani Bukombe mkoani Geita  ambapo amekuwa akitoa huduma ya kutibu
Moyo  kwa watu wazima na watoto.
Profesa
Mahalu  amesema   wazazi wengi hawatambui matatizo ya moyo kwa
watoto wao kwani hospitalini hapo amekuwa akiwatibu watu wengi  kwa mwezi 
wagonjwa  wenye matatizo ya moyo
ni  77 hadi 80   kati yao watoto ni asilimia 5.
“Wazazi
wengi hawatambui  magonjwa  ya moyo kwa watoto wao wengi wanafikiri mtoto
anakikohozi nakumpeleka kwenye vituo vya afya au zahanati hawafikirii kuwapatia
vipimo ili kubaini tatizo mapema”alisema profess Mahalu.
Profesa  Mahalu amesema  magonjwa ya kuridhi  mfano shinikizo la damu  mengine yakuyapata  kutokana 
na desturi ya vyakula vinavyoliwa kwa 
kuwekewa mafuta mengi  nakufanya
moyo kutanuka na wengine kuzaliwa  moyo
na matundu.
“Zamani
walikuwa na imani za kishirikina lakini sio kwamba siku hizi magonjwa mengi
bali yametambuliwa  mengi na kufanyiwa
mchakato wa kupata tiba yake”amesema 
profesa Mahalu.
Profesa
Mahalu amesema   bado watu wanatumia ulaji
wa chumvi  usio na utaratibu  mzuri nao ni changamoto inayoleta madhara katika
moyo ushauri waepuke ili kuondoa madhara hayo.
‘Wagonjwa
wengi walikuwa wakishindwa kusafiri kwenda Mwanza kupata matibabu ya Moyo  lakini hospitali ya Charles Kulwa Memorial  imeweza kusogeza huduma hii kwa ukaribu.”amesema  profesa Mahalu.
Mkurugenzi
wa hospitali ya Charles  Kulwa Memorial  dkt  Baraka Kulwa 
anasema  kwa sasa  wamekuwa wakitoa  huduma za kibingwa  kila siku na madaktari wapo zamani ilikuwa
mara moja kwa mwezi.
Kulwa
anasema wagonjwa wamekuwa wakiongezeka kutoka maeneo mbalimbali wenye bima za
afya  na wasiokuwa nazo  kwani kiwango wanachokitoa ni kama hospitali
ya wilaya na sasa wanataka kupigania ifike kiwango cha mkoa.
Dkt Kulwa
amesema  serikali imeweka mazingira
mazuri kwa ushirikiano wa kutoa baadhi ya dawa na vifaa tiba bure kwa lengo la
kutoa huduma ya kliniki  kwa baba,mama na mtoto.
Baadhi ya
magonjwa dawa zake tunapewa bure na serikali mojawapo ni kifua kikuu,  ukoma ,huduma za
CTC  na huduma ya kliniki ya baba na
mtoto (RCH) bure kwani vifaa tiba serikali inatoa ili kuokoa vifo vya mama na
mtoto pia .
Mtaalamu wa  masuala ya mionzi (Utralsaound)  kutoka hospitali ya Charles Kulwa
Memorial  Elmil  Mmanyi anawashauri   wajawazito   mimba inapofikisha
 umri  wa miezi 20  wapate kuchunguzwa waangaliwe  vinasaba vya  mtoto kuzuia asipatwe na  matatizo ya mdomo sungura,kichwa kikubwa,moyo
 na mgongo wazi .
Mmanyi
amesema  wapo wajawazito waliofika hapo
na kubainika watoto wao waliopo tumboni wana changamoto lakini  ilivyobainika 
walianza kupata huduma na tatizo hilo likaondoka.
Mtaalamu wa Mionzi bingwa kutoka hospiatli ya rufaa Bugando Rajabu Kidenda anayetoa huduma kwenye hospitali ya Charles Kulwa Memorial anasema kuwa Utralsound ni mionzi iliyosalama .
 Pia kwa siku katika hospitali hiyo huwafanyia
watu 30 hadi 40 wakiwemo wajawazito  na
wiki moja hutoa elimu mara mbili juu  mionzi hiyo.






Mtaalamu wa maabara Yusuph Hashimu akiwa kazini katika hospitali ya Charles Kulwa Memorial




Mtaalamu wa mionzi (ultrasound) kutoka hospitali ya rufaa ya Bugando Rajabu Kidenda akiwa katika hospitali ya Charles Kulwa Memoriali akitoa huduma. Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464
 
 
       
 
 
