Mtaalamu wa wanyapori kutoa Dar'es-salaam akimueleza mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Kahama Charles Lutonja namna ambavyo wanautangaza utalii kwa hifadhi ya wanyapori inayotembea
Na Kareny Masasy, Kahama
JUMUIYA ya wazazi ya chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imeadhimisha kumbukizi ya kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuhamasisha wananchi kutembelea wanyamapori .
Mwenyekiti
wa jumuiya ya wazazi wilaya ya
Kahama Charles Lutonja amesema hayo kwenye ufunguzi wa maonyesho ya biashara na
uhifadhi wa wanyama pori unaotembea
unaofanyika kwenye viwanja vya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Lutonja
amesema wameamua kuadhimisha kuanzia tarehe
14/10/2022 hadi tarehe
22/10/2022 kwa kuendeleza kupinga
mambo matatu ya ujinga,maradhi na
umasikini sanjari na kuutangaza utalii
wa ndani.
Lutonja
amesema Marais wote waliopita na Rais wa
sasa wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan ambaye anaendelea kupigania
watanzania wapate elimu ndiyo maana ameleta fedha tena kwaajili ya ujenzi wa
vyumba vya madarasa.
Lutonja amewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata
elimu na kutokomeza mimba za utotoni na kuwasimamia vijana wasikae hovyo
vijiweni nakujifunza mambo mabaya.
“Ilani ya
chama cha Mapinduzi inayotekelezwa na serikali imefanya mambo makubwa ya kuleta
maendeleo ukiangalia suala la elimu
bure lengo watoto wote wapate elimu
na kama taifa watu wake wakiwa wajinga
hakuna maendeleo yatakayofanyika”amesema Lutonja..
Mjumbe wa
baraza la wazazi Taifa Hatibu Mgeja
amesema Hayati mwalimu Nyerere alipigana
na maadui watatu na kila mwaka yanaenda yakibadilika kwani kuna vituo vingi vya afya vimejengwa,
sekta ya elimu vyumba vya madarasa na
pongezi hizi ziende kwa Rais Samia Suluhu
kwa kutekeleza kwa vitendo.
Katibu wa
chama cha Mapinduzi wilaya ya Kahama
Mary Muhoha amesema leo
kumbukumbu ya baba wa taifa wameamua kuutangaza pia utalii wa ndani kwa
kuwaleta wanyama ili wananchi wajifunze
na kuwaona na kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi.
“Tunautangaza
utalii wetu kwa kumsaidia Rais kwani
unaingiza pato la taifa na kunyanyua
uchumi wengi wamekuwa wakishindwa kwenda
Mbuga za wanyama lakini leo wameletewa hapa hapa na kuchangi sh 1000 wadogo na wakubwa 2000 tofauti ambavyo wangeenda Serengeti au Mikumi
wangetoa pesa nyingi”. amesema Muhoha
Katibu Muhoha amewataka wajasiriamali kutumia fursa ya kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi kupata maarifa ya kujiongezea kipato kwani taasisi 14 muhimu zenye mrengo tofauti ziko hapa zinatoa elimu.
Viongozi wa jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi wakiwa na katibu wa chama hicho wilaya ya Kahama katika ofisi za uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Mwenyekiti wa jumuya ya wazazi wilaya ya Kahama Charles Lutonja akipatiwa maelezo na mtaalamu wa wanyapori.
Viongozi wa jumuiya ya wazazi wilayani Kahama wakiangalia wanyamapori katika banda walilohifadhiwa simba.
Mwenyekiti wa wanawake wa uwezeshaji wananchi kiuchumi mkoani Shinyanga Regina Malima akiwaelezea viongozi namna ya mamalishe wanavyojinyanyua kiuchumi.
Mwakilishi wa baraza la wazazi taifa kutoka wilayani Kahama Hatibu Mgeja akisalimia wananchi katika kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi.
katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Mary Muhoha akiongea namna ya kupatikana kwa fursa kwenye kituo cha uwezeshaji wananchi na kuhamaisha utalii wa ndani.
0 Comments