Header Ads Widget

MERY MAKAMBA ATOA MCHANGO WA MAJI KATIKA MSIKITI WA IJUMAA KWA AJILI YA KUTUMIA SHEREHE YA MAULID


Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Mery Makamba ametoa mchango wa maji katika msikiti mkuu wa Ijumaa kwa ajili ya Maulid

Suzy Luhende,Shinyanga Blog

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Mery Makamba ametoa katoni 30 za maji katika msikiti mkuu wa Ijumaa kwa ajili ya kutumia katika sherehe ya Maulid itakayofanyika Oktoba 22,2022.

Makamba amesema ameguswa kuchangia maji katoni 30 yenye thamani ya Sh 95000, ambayo yatawasaidia kutumia katika sherehe ya maulidi itakayo fanyika oktoba 22,mwaka huu.


"Nimeguswa kutoa maji kwa ndugu zangu ili kuweza kufanikisha sherehe hii ya Iddi itakayofanyika hivi karibuni,nimeona tusherehekee pamoja kwa sababu ni wamoja, amesema mjumbe wa kamati ya utekelezaji Mery Makamba.


Akitoa shukrani baada ya kukabidhiwa maji hayo katibu wa shekhe wa Wilaya Abdalah Abasi, anamshukuru sana kwa kujitolea, hivyo aendelee na moyo huo huo na Mungu ambariki kwa kuwakumbuka.

"Sherehe yetu inafanyika oktoba 22 mwaka huu, hivyo tunashukuru kwa msaada huu tunamuombea mama huyu pale alipotowa Mungu amzidishie, tunamtakia la kheri"amesema Abasi.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini  Mery Makamba akizungumza baada ya kukabidhi maji hayo.

Mery Makamaba akizungumza baada ya kutoa mchago wa maji katika msikiti wa Ijumaa kwa ajili ya Maulid.

Katibu wa shekhe wa Wilaya Abdalah Abasi, akiwa na mjumbe wake wakishukuru kwa kuchangiwa maji hayo.

Katibu wa shekhe wa Wilaya Abdalah Abasi, akishukuru kwa mchango huo
Mjumbe wa msikiti mkuu wa ijumaa Ramadhan Majani akimshukuru  Mery Makamba kwa mchango huo.

Mery Makamba akikabidhi maji hayo.

Post a Comment

0 Comments