Header Ads Widget

KUTOKANA NA WANANCHI WA MKOA WA SHINYANGA KUWA NA CHANGAMOTO KUBWA YA UGONJWA WA MACHO, MADAKTARI WAKUBALI KUONGEZA SIKU MOJA KUENDELEA NA UPASUAJI WA MACHO


Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission Of Tanzania Free Eye Camp, ambaye pia ni kiongozi wa jopo la madaktari  bingwa wa macho Ain Sharif,akizungumza jinsi ya kuwahudumia wananchi .

Suzy Luhende, Shinyanga blog 

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga amesema kutokana na changamoto ya uwepo wa watu wengi wenye matatizo ya macho mkoa wa Shinyanga, amekaa na madaktari na kuwaomba waongeze siku moja ili waweze kuhudumia wananchi ambao bado hawajahudumiwa, hasa wale wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji wa macho.

Hayo ameyasema jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga, ambapo amesema kulingana na  watu wengi wa mkoa wa Shinyanga kuwa na changamoto kubwa ya macho ameona akae na madaktari waongeze siku ili watu wenye matatizo ya kupasuliwa macho wapasuliwe.

"Kweli Shinyanga nimeona kuna shida kubwa ya macho, hivyo nawaomba wale ambao watahudumiwa kwa kupewa dawa na kupewa miwani huduma yao itaishia leo jumapili na wale wa kufanyiwa upasuaji wataendelea mpaka kesho jumatatu ndipo madaktari wetu wataondoka jumanne kwenda kuendelea na shughuli zao"amesema Lucy Mayenga.

Baadhi ya wananchi waliokuwa wamehudumiwa Felister Bundala na Elias Shija kutoka Kishapu wamesema wanamshukuru sana mbunge kwa kuwaletea huduma hiyo kwani walikuwa hawaoni vizuri wakati wa kusoma, lakini baada ya kufanyiwa matibabu tena ya bule bila malipo wanaona.

"Baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa kutakuwa na huduma hii nimesafiri kutoka Kishapu kuja kuhudumiwa, nimepata Miwani naona vizuri, hivyo ninashukuru sana maana nilikosa fedha ya kulipia ili nitibiwe, lakini hospitalini lakini mbunge wetu Lucy Mayenga ametukumbuka  kwa sasa nimetibiwa bure kabisa sijatoa shilingi yeyote hivyo tunawaomba na wabunge wengine waige mfano wa Lucy Mayenga"amesema Elias Shija.

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga, ambaye na yeye alifika kwenye viwanja vya Shycom kwa ajili ya kuhudumiwa macho amesema kutokana na wingi wa watu inaonyesha kuwa tatizo la ugonjwa wa macho kwa mkoa wa Shinyanga ni kubwa, na hii ndio kutekeleza wa ilani ya chama cha mapinduzi  CCM  kwamba viongozi watatoa huduma kulingana na wanavyofanikiwa.

Naye Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission Of Tanzania Free eye Camp, ambaye pia ni kiongozi wa jopo la madaktari hao bingwa wa macho Ain Sharif,  amesema madaktari hao bingwa wa macho kuwa wanatoka katika Hospitali ya KCMC, AGHAKHAN, Mhimbili, Hindu na Madali na kwamba taasisi yao wanashirikiana na shirika la uingereza kwa ajili ya kuhudumia jamii.

"Mheshimiwa mbunge Lucy Mayenga alituomba tuje kuhudumia wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa muda wa siku tatu, lakini kulingana na ongezeko la watu mbunge ametuomba tena tuongeze  siku moja ili tuwahudumie wananchi, ambao bado hawajahudumiwa"amesema Sharif.

" Wakati tunakuja Shinyanga hatukutegemea kama hali itakuwa hivi, lakini baada ya kuanza matibabu watu wanazidi kuongezeka  kufikia leo tumehudumia watu zaidi ya 4000, hivyo kufikia kesho wataongezeka kutokana na tatizo kuonekana kubwa ndiyo maana tumeona tukubali tuongeze siku moja nyingine ya juma tatu ili wale wa kufanyiwa upasuaji wa macho waendelee kuhudumiwa, lakini wale wa huduma ya kawaida tutaishia leo, tutapanga tena siku nyingine tuje"amesema Dkt.Ain Sharif.

Kwa upande wake Dkt. Joseph Kimati kutoka kitengo cha macho  hospitali ya mkoa wa Shinyanga, amesema tatizo la macho ni kubwa sana wahitaji ni wengi kufikia kesho watakuwa zaidi ya 7,000  na ni vizuri serikali ikatilia mkazo suala la macho iendelee kutafuta wafadhili wa macho, kwani wataalamu kwa mkoa mzima wapo wanne tu ndio maana wengi wana shida ya macho.

Wananchi wakiendlea kupatiwa huduma katika chuo cha Shycom

Wananchi wakisubiri kuhudumiwa

Mmoja wa wananchi akiendelea Matibabu  

huduma zikiendelea kwa wananchi wenye matatizo ya macho
Mwananchi akifanyiwa vipimo 

Dkt. Joseph Kimati kutoka kitengo cha macho hospitali ya mkoa akiendelea na matibabu ya macho

Wananchi wakiwa eneo la matibabu wakisubiri kitibiwa,


Matibabu ya macho yakiendelea.

Post a Comment

0 Comments