Header Ads Widget

MIONZI YA JUA NI KIKWAZO KWA WENYE UALBIONO KUKUA KIUCHUMI NDANI YA JAMII

 

MIOZI YA JUA KIKWAZO KWA WENYE UALBINO KUKUA KIUCHUMI NDANI YA JAMII

 


Watoto wenye Ualbino wakiwa wameshika Lotion ambao watazitumia kwa ajili ya kulinda ngozi za0.


Watoto wenye Ualbino wakiwa wameshika Lotion ambao watazitumia kwa ajili ya kulinda ngozi zao.

  

Na Shaban Njia,Kahama

 

MOJA ya sababu inayowafanya watu wenye Albino kushindwa kujishughulisha katika shughuli za uzalishaji mali inatokana na kushindwa kukaa juani kwa muda mrefu kutokana na ngozi zao kuharibiwa na mionzi ya jua hali inayofanya kufanyakazi kwa muda mfupi sana.

 

Wakati wa msimu wa kilimo wanalazimika kulima kuanzia majira ya saa moja kamili mpaka saa tatu asubuhi kabla ya jua kuanza kuwa kali kwani ngozi zao hazina uwezo wa kuhimili jua,hali inayofanya kuzalisha mazao ya chakula na biashara kwa uchache ukilinganisha na watu wengine.

 

Aidha,kutokana na hali hiyo wafanyabishara wengi wenye Albino wanalazimika kufanyakazi sehemu moja kwenye kimvuli kutokana na kushindwa kuzunguka kama walivyo watu wengine,hatua ambayo inawafanya wafanyabiashara wenye ulemavu huo kuwa wachache nchini.

 

Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ualbino (TAS) Nisha Phabiani alitoa ombi hilo jana wakati akieleza namna ambavyo wamekuwa wakishirikiana moja kwa moja katika shughuli za kiuchumi licha ya kusumbuliwa na jua mara kwa mara.

 

Alisema, kutokana na hali hiyo wengi wao waliofanikiwa kimaisha kwa kupata nyadhifa mbalimbali serikali na taasisi binafsi,wamekuwa wakiwasaidia kulingana na uwezo wao hali ambayo baadhi yao wanafaidika na wengi wanakosa kutokana na kuishi pembezoni mwa miji.

 

“Kuna wenzetu wengi wamefanikiwa kama vile Haji Sunday Manara na Abdallah Possi ambae kwasasa ni Balozi nchini Ujerumani, wamekuwa msaada mkubwa kwetu kwa kutusaidia vitu mbalimbali lakini kutokana na kundi kuwa kubwa baadhi yetu waliokaribu wananufaika kupitia viongozi hao”Alisisitiza Phabiani.

 

Hata hivyo alisema, hawabagui kazi yoyote kulingana na udhaifu wao walionao na badala yake wamekuwa wakifanya kila kazi za kuwaingizia kipato lakini changamoto ya miili yao inawafanya kufanya kazi kwa muda mfupi hali inayowafanya kutotumiza malengo yao ya kiuchumi kwa wakati.

 

Nae Gasper Wiiliamu,mwenye ualbino anayeishi kata ya Segese Halmashauri ya Msalala alisema, amekuwa akifanyakazi za kujiingizia kipato nyakati za asubuhi kabla ya jua kuwa kali na linapokuwa kali analazimika kuendelea na kazi jioni mpaka saa mbilui usiku na kurejea nyumbani.

 

Mwingine George Maziku mkazi wa kagongwa Manisaa ya Kahama alisema, kazi zake nyingi amekuwa akizifanya kinvulini na zile anazolazimika kuzifanya juani analazimika kushirikiana na wasiokuwa na tatizo kama lake na kujiingizia kipato kwa sababu wanatambua hali yake.

 

 

 

Post a Comment

0 Comments