Header Ads Widget

KAMATI YA UKUSANYAJI MAPATO MANISPAA YA SHINYANGA YAENDELEA NA ZIARA KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO ITOKANAYO NA MCHANGO WA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI

Kamati ikiwa kwenye mradi ujenzi wa Zahanati Seseko.

Kamati ikiendelea kuangalia miradi ya maendeleo itokanayo na fedha za mapato ya ndani.

Na Mwandishi Wetu

Kamati ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, imefanya ziara kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inatokana na mchango wa fedha za mapato ya ndani.

Ziara hiyo imefanyika jana ikiwa ni muendelezo wa ziara za kamati hiyo ambapo wametembelea miradi mitano ukiwamo wa Zahanati ya Bushola, Seseko, Masekelo, Mwasele, ujenzi wa Maabara ya Sanyansi Shule ya Sekondari Mwamalili, pamoja na Shule ya Wasichana ya Sekondari iliyopo Butengwa Kata ya Ndembezi.

Katibu wa Kamati hiyo Dk. Kulwa Meshack akizungumza kwenye ziara hiyo ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kwa kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu Itokanayo na mchango wa fedha za mapato ya ndani.

“Kamati tulikubaliana kwanza tuanze na kukusanya mapato halafu pili mapato yale asilimia 60 fedha zake zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo, lakini Mkurugenzi akaona aongeze asilimia 10 kwa ajili ya kuboresha miradi mbalimbali ya halmashauri, na asilimia 30 zilizobaki ziende kwenye shughuli za kiutawala, na sasa tunaona mapinduzi makubwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye manispaa yetu”amesema Dk. Meshack

“Tunaona namna miradi hii inavyotekelezwa na kuleta tija kwa wananchi ikiwamo kwenye sekta ya afya na elimu na sisi kama kamati ya ukusanyaji mapato tunaendelea kuhamasisha ukusanyaji wa mapato,”ameongeza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa Shinyanga Jomaary Satura amesema utekelezaji wa miradi hiyo unaenda sambamba kulingana na ukusanyaji wa mapato ya ndani, na wananchi wanaona namna mapato wanayolipa yanavyosaidia katika kuleta maendeleo.

Post a Comment

0 Comments