Header Ads Widget

EWURA YAWAPIGA MSASA MAFUNDI UMEME, DC MBONEKO AKEMEA MATUMIZI YA VISHOKA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati akifungua mafunzo ya mafundi umeme na EWURA.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAMLAKA ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendesha mafunzo ya siku mbili kwa mafundi wafungaji wa miundombinu ya umeme kwenye majengo, ili wafanye kazi zao kwa ufanisi na kuepuka majanga ya moto yatokanayo na hitilafu ya umeme.

 
Mafunzo hayo yameanza kutolewa leo Oktoba 12, 2022 Mjini Shinyanga na yatahimishwa kesho, ambayo yameshirikisha mafundi umeme kutoka Mikoa minne ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Geita, Mwanza, Simiyu na wenyeji Shinyanga.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa George Mhina, amesema wameendesha mafunzo hayo kwa mafundi umeme ili kuongeza ufanisi wa utendaji wao kazi, ambapo hivi karibu kume kuwepo na majanga mengi ya moto kwenye majengo, na chanzo chake mara nyingi kikifuatiliwa ni hitilafu ya umeme.

“Tusipo wazingatia mafundi hawa tunaweza kupata majanga mengi ya Moto sababu ya ufanyaji wa kazi bila ya ufanisi, aidha kwa kufunga mifumo ya umeme na nyaya zisizo imara kwenye majengo bila ya kuzingatia ubora, na matokeo yake nyumba nyingi kuzidi kuungua Moto,”amesema Mhina.

Pia, amewataka mafundi hao wa umeme wawe na bei moja na rafiki kwa wateja wao, na kuacha kila mmoja kuwa na bei yake ambayo inaumiza wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amewataka mafunzi hao wazingatie mafunzo ambayo wanapewa na EWURA pamoja na kutanguliza uzalendo mbele na kuacha kufanya kazi chini ya kiwango.

“Nawaombeni mafundi umeme mtangulize uzalendo mbele, na kufungia watu umeme kwenye majumba yao pamoja na majengo ya Serikali vifaa imara vya umeme, na siyo kuweka nyaya mbovu na kusababisha majanga ya moto kuendelea kutokea na kuwatia hasara wananchi na hata kusababisha vifo,”amesema Mboneko.

Pia amewataka wananchi wanapokuwa wakitaka kufunga mifumo ya umeme majumbani mwao wasitumie mafundi umeme ambao ni vishoka, bali watumie wale ambao wamesajiliwa na wana Leseni ili kuepuka kufungiwa mifumo mibovu ya umeme na kusababisha majanga ya moto.

Katika hatua nyingine Mboneko, amelitaka Shirila la Umeme Tanzania (TANESCO) wanapokuwa katika majukumu yao ya kusambaza umeme kwa wananchi, wasitumie mafundi umeme ambao ni vishoka, ili umeme ambao unapelekwa kwa wananchi usilete madhara.

Baadi ya mafundi hao umeme akiwamo Lucy James, wamepongeza kupewa mafunzo hayo ambayo yatawaongezea ufanisi katika utendaji wao kazi.  
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati akifungua mafunzo ya mafundi umeme na EWURA.


Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa George Mhina akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya mafundi umeme.

Fundi umeme Lucy James kutoka Shinyanga akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akimkabidhi Lesseni ya ufundi umeme Charles Jackson kwenye mafunzo hayo.

Mafundi umeme wakiwa kwenye mafunzo na EWURA.

Mafundi umeme wakiwa kwenye mafunzo na EWURA.

Mafundi umeme wakiwa kwenye mafunzo na EWURA.

Mafundi umeme wakiwa kwenye mafunzo na EWURA.

Mafundi umeme wakiwa kwenye mafunzo na EWURA.

Mafundi umeme wakiwa kwenye mafunzo na EWURA.

Mafundi umeme wakiwa kwenye mafunzo na EWURA.

Mafundi umeme wakiwa kwenye mafunzo na EWURA.

Picha ya pamoja ikipigwa kwenye mafunzo hayo.

Picha ya pamoja ikipigwa kwenye mafunzoi hayo.

Post a Comment

0 Comments