Header Ads Widget

UWT SHINYANGA MJINI YAALIKA WAJUMBE WA MKUTANO UCHAGUZI


Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga,Lucy Enock akizungumza na Shinyanga Press club blog.


Na Suzy Luhende, Shinyanga

Katibu wa umoja wa wanawake UWT wilaya ya Shinyanga Lucy John Enock anawakaribisha wajumbe wote wa UWT wilaya kwenye mkutano wa uchaguzi utakaofanyika tarehe 24,9,2022 utakaofanyika katika ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini.


Katibu ametoa wito huo leo wakati akizungumza na Shinyanga Press club Blog, ambapo amesema wajumbe wote wa UWT wilaya wanatakiwa kufika katika ukumbi huo tarehe 24/9/2022 kuanzia saa 2: 00 asubuhi ili kuja kufanikisha uchaguzi huo.


" Ili kuwapata viongozi wa UWT wilaya wajumbe wote mnatakiwa kufika kwa wakati, na uchaguzi huu ni mwendelezo wa uchaguzi wa chama cha mapinduzi CCM na jumuia zake, hivyo unaombwa kuhudhulia Mkutano huo bila kukosa",amesisitiza Lucy.


Pia wajumbe wote wanakumbushwa kuja kwenye mkutano huo wakiwa wamevaa sare ikiwa ni pamoja na wagombea wote.

Post a Comment

0 Comments