Header Ads Widget

MUUGUZI WA HOSPITALI KORTINI TUHUMA ZA KUBAKA NA KULAWITI MTOTO ALIYEKUWA AKIMPATIA MATIBABU

Muuguzi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Amana jijini Dar es Salaam, Joseph Mwaipola (50) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka matatu, yakiwemo ya kubaka na kulawiti mtoto wa miaka 17, ambaye alikuwa ana mtibu.

Mwaipola amefikishwa mahakamani hapo, leo Ijumaa Septemba 9, 2022 na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali Mwandamizi, Slyvia Mitanto mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Ruboroga.

Katika mashtaka yao, Mwaipola anadaiwa Februari 2022 katika Hospitali ya Rufaa ya Amana, iliyopo wilaya ya Ilala, alimbaka na kumlawiti binti wa miaka 17, kinyume cha sheria.
 
SOMA HAPA ZAIDI  CHANZO MWANANCHI

Post a Comment

0 Comments