Header Ads Widget

MKURUGENZI WA SHULE ZA ROCKEN HILL ACADEMY NA ANDERLEK RIDGES AMETAKA WATOTO WAPEWE ELIMU DUNIA IMEBADILIKA.
Mkurugenzi mkuu wa shule ya msingi Rocken Hill Academy na Anderlerk Ridges Alexander Kazimili akitoa hotuba mbele ya wazazi na wafunzi waliohudhuria mahafali ya shule hizo mbili kwa darasa la saba na kidato cha nne

Na Kareny Masasy,   Kahama

MKURUGENZI Alexander Kazimili wa shule ya msingi Reckon hill Academy na Anderlek Ridges zilizoko wilayani Kahama mkoani Shinyanga amewataka wazazi kuwasomesha watoto wao kwa bidii kwani elimu ndiyo moyo wa dunia ikiwa nchi kama watu wake hawajasoma hakuna maendeleo.

Mkurugenzi Kazimili ameyasema hayo leo tarehe 16/09/2022 katika mahafali ya 18 ya shule ya msingi Rocken Hill Academy ikiwa imeambatana na mahafali ya kidato cha nne kwa siku moja nakufanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Anderlek. Huku mgeni rasmi akiwa meneja wa benk ya CRDB tawi la Kahama Evodi Kereti

Mkurugenzi Kazimili amesema kuwa umasikini wa fikra ni mbaya sana kuliko umasikini wa kipato hivyo elimu ndiyo msingi wa kila kitu hapa duniani ambapo amewataka wahitimu hasa kidato cha nne kwenda kuyatumia maarifa ya elimu na maadili huko mitaani waendako.

“Ninafuraha sana kuletewa watoto na kuwalea kwani ninyi wazazi mmeniamini sana kuwa mlezi wa watoto wenu na mimi natumia maarifa mengi kuhakikisha watoto mlioniletea hawaendi kinyume na maadili nakufanya vizuri katika masomo yao" amesema Kazimili

.Kazimili amesema kuwa elimu lazima iheshimiwe kwa kila namna na watoto wasichezee elimu wanaoipata na malengo makubwa ya elimu ni kuleta mapinduzi ya kifkra ndivyo wanavyotaka vijana wabadilike na kuleta maono yao kulisaidia taifa.

“Sasa hivi ajira imekuwa ngumu hivyo vipaji vina fursa kubwa ndiyo maana shuleni hapa kuna taaluma ya kukuza vipaji nakuwataka wazazi wawaangalie watoto wao tangu wakiwa wadogo wanapendelea nini sababu kipaji chake ndiyo kitamkomboa katika maisha yake ya baadaye” Kazimili..

Mkurugenzi wa shule ya msingi Rocken Hill  Academy Ephraim  Edward  Kabeya amesema kuwa shule hiyo ina wahitimu 154 wa darasa la saba  ikiwa wasichana  81 na wavulana 73 ambapo tayari wamejiandaa vyema kwa mitihani ijayo huku akieleza kuwa wamekuwa wakifanya vizuri kila mwaka na kuingia nafasi ya kumi bora kitaifa.

Mkurugenzi wa shule ya sekondari Anderlek Ridges Marco Shigele amesema kuwa wanafunzi wa kidato cha nne wameandaliwa vizuri wako tayari kwa mitihani ambapo wahitimu 180 wanatarajia kufanya mitihani kwa mwaka huu.

“Upande wa sekondari tumekuwa tukifanya vizuri kwa mwaka jana walifanya mtihani wanafunzi 205 na wanafunzi 192 walichaguliwa moja kwa moja kwenda kidato cha tano na wengine chuo sawa na asilimia 93.7”amesema mwalimu Shigele

Wanafunzi wa darasa la saba ambao ni wahitimu kutoka shule ya msingi Rockeni Hill Academy
Mgeni rasmi ambaye ni meneja wa benki ya CRDB tawi la Kahama Evodi Kereti akitoa hotuba katika mahafali ya kidato cha nne na darasa la sabaBaadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Anderlek wakitumbuiza kwa furaha jukwaani

Wanafunzi wa kidato cha nne ambao ni wahitimu kutoka shule ya sekondari Anderlek wakiangalia burundani mbalimbali

Wageni wa waalikwa na mgeni rasmi wakiwa meza kuu.

Wanafunzi ambao wapo kitengo cha skauti shule ya msingi Rocken Hill wakiwa wamekaa baada ya kumvika skafu mgeni rasmi.

Wanafunzi wa shule ya msingi Rocken Hill Academy wakionyesha vipaji vyao jukwaani kwa kucheza
Wanafunzi wakitumbuiza ngoma ya asili kwa kuonyesha vipaji vyao.
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa jukwaani wakicheza nyimbo ya mahafali ya kidato cha nne na shule ya msingi.

Wahitimu wa darasa la saba wakiimba na kufurahia mahafali yao
Wahitimu wa kidato cha nne wakiwa jukwaani wakicheza kwa kufurahia kuhitimu

Mkurugenzi wa shule ya sekondari ya Anderlek Ridges Marco Shigele akitoa taarifa juu ya shule hiyoMkurugenzi wa shule ya msingi Rocken Hill Academy Ephraim Edward  Kabeya alisoma taarifa juu ya shule hiyo

Wanafunzi wa shule ya msingi Rocken Hill Academy wakicheza jukwaani.
Wahitimu watarajiwa wa darasa la saba shule ya  Msingi  Rocken Hill Academy

Post a Comment

0 Comments