Header Ads Widget

MKURUGENZI HALMASHAURI YA IGUNGA FATUMA LATU AFARIKI AJALI YA GARI

DED Igunga afariki ajalini Mbeya

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatuma Latu amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari katika eneo la Inyala, Mbeya. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatuma Latu amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari katika eneo la Inyala, Mbeya.
 
Ajali hiyo imetokea leo Jumatano, Septemba 14, 2022 wakati akiwa anatoka kwenye kikao cha Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) jijini Mbeya.

Akizungumzia ajali hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Igunga, Lucas Bugota amethibitisha kutokea kifo hicho.

Bugota amesema kuwa walikuwa wote kwenye safari lakini kwenye magari tofauti.

"Mi ndio naelekea huko kwani wao walikuwa nyuma yetu, yaani ndio hivyo tumepata msiba" amesema.
 
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments