Header Ads Widget

MAMA AKIWA MJAMZITO NA KUMUACHISHA MTOTO AKIWA UMRI MDOGO HUKO NI KUMTESA NA KUMLETEA MADHARA.

Wazazi wakiwa  kwenye Zahanati ya Ntobo halmashauri ya Msalala wakipatiwa elimu  juu ya unyonyeshaji kwa watoto ili kuwaepusha na maradhi.

Na Kareny Masasy, Kahama

DAKTARI bingwa wa  magonjwa ya watoto  kutoka hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga  dk Mwita Ngutunyi amesema kuwa mila na desturi za kumuachisha mtoto maziwa ya mama pale anapokuwa  mama mjamzito   kwa madai yataleta madhara inawatesa watoto.

Dk Ngutunyi ameyasema  hayo jana katika mada ya hali ya lishe na huduma kwa watoto  alipokuwa kwenye mafunzo ya wataalamu wa afya, maafisa lishe na ustawi wa jamii  kutoka kanda ya ziwa iliyojumuisha mikoa mitano ya  Mara,Mwanza,Simiyu Geita na Shinyanga

“Mila ya kumuachisha mtoto akiwa na miezi kadhaa wakati mama akiwa mjamzito ni hatari  inasumbua  hivyo wazazi wanaweza kutumia mbinu ya uzazi wa mpango kupangilia ili watoto wao waendelee kuwa na afya nzuri na  mzazi arudishe afya yake”amesema Ngutunyi..

Dkt Ngutunyi alisema  kuwa wazazi wasipotumia uzazi wa mpango  mtoto hata ukuaji wake unakuwa sio mzuri na kumrudisha mtoto kukaa kwenye hali yake  huwa ni ngumu na gharama ni kubwa hivyo ujauzito unatakiwa upatikane kwa mpango.

Dk Ngutunyi amesema  kuwa lengo la mafunzo ni kuainisha  vitu vinavyosababisha  utapiamlo  ambao wakuzidisha  chakula  haupo sana kwa watoto na upo ule  wa ukosefu wa lishe yenye mpangilio unaohitajika.

“ukosefu wa madini ya vitamin A  utamfanya mtoto kuwa na uoni hafifu au kutokuona kabisa na  ukosefu wa madini chuma  unachangia upungufu wa damu mwilini  na  madini joto unamfanya mtoto kutokukua vizuri”amesema  Ngutunyi.

Ofisa lishe mkoa wa Shinyanga Denis Madeleka amesema  kuwa  asilimia 71 ya watoto chini ya umri wa miaka mitano  mkoani Shinyanga wanaupungufu wa damu  ikiwa baadhi ya wazazi wamekuwa hawanyonyeshi kwa utaratibu unaotakiwa maziwa ya mama ambayo yana virutubishi vingi.

Baadhi ya maafisa lishe  Bundi Clemet na Peter Shimba  wamesema  kuwa mama akiwa mjamzito anapaswa kunyonyesha  kwa kipindi cha umri wa mimba yake ikifika  miezi saba  hakuna madhara na wengi huwakatisha hasa wakiwa na ujauzito  nakuwatenga.

Post a Comment

0 Comments