Header Ads Widget

WATU WENYE ULEMAVU WASIFICHWE WASHIRIKI KUHESABIWA SENSA

 

Mwenyekiti wa CHAWATA Mkoa wa Shinyanga Mohamed Ally

 NA HALIMA KHOYA, SHINYANGA.

CHAMA Cha walemavu Tanzania (CHAWATA) Mkoani Shinyanga, kimewataka wazazi na walezi ambao ni wakuu wakaya, kushirikiana kikamilifu na Makarani wa Sensa na kutoa taarifa sahihi, itakayo isaidia Serikali kupanga mipango yao na kuwatimizia mahiaji yao.

 

Akizungumza hayo jana katika kikao cha Halmashauri ya Wilaya Shinyanga Katibu wa CHAWATA Mkoa, Daudi Nyahiti  katika kikao kilichowakutanisha Viongozi wote katika Mkoa huo ambacho ajenda kuu ni kuhamasisha Sensa ya watu na makazi, kwa watu wenye ulemavu.

Katibu huyo amewataka Wana Kaya wote za watu wenye ulemavu kutumia ipasavyo elimu waliyopatiwa kuelekea katika zoezi hilo na kujiamini, hali  itakayopelekea kutoa majibu sahihi ya maswali watakavyo ulizwa pamoja na changamoto zinazowakabili ili kuifanya serikali kutimiza majukumu yake ipasavyo.

"Wazazi na walezi wote wenye walemavu sisi kama uongozi tunawaasa kujiamini na kutumia elimu ipasavyo ili kutoa taarifa sahihi ambazo zitasaidia serikali kuwakomboa kwa kuwaletea  Baadhi ya mahitaji muhimu ya walemavu(Viti mwendo), amesema Nyahiti.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHAWATA ,Masanja Magasa, ameeleza jinsi wanavyotoa elimu kwa Baadhi ya vijiji vilivyopo ndani ya Wilaya na kubainisha kuwa wapo Makatibu katika kila kata ikiwa kazi yao kubwa ni kuhamasisha Sensa kwa walemavu hao ili kujipatia haki zao za msingi kama raia katika Nchi hii.

Aidha, Mwenyekiti wa CHAWATA Mkoa Mohamed Ally, amewashauri Makarani hao wawe na kauli nzuri kwa walemavu pamoja na kuwavumilia wawapo katika Kaya hizo ili kuepusha mkanganyiko wa kauli kati yao.

Vile vile Mwenyekiti amesisitiza uzalendo kwa wakuu wa Kaya kwa kutoa taarifa sahihi na kukanusha kauli isemayo "Ulemavu ni ugonjwa jambo lisilo na ukweli ndani yake na kubainisha kuwa ulemavu hutokea kwa mipango ya Mungu.

 Zoezi la kuhesabu Sensa ya watu na Makazi lilianza Agosti 23 mwaka huu na litakwenda hadi Agosti 28.

Post a Comment

0 Comments