Header Ads Widget

WANANCHI -SHINYANGA WALALAMIKA KUPANDA KWA NAULI ZA VYOMBO VYA USAFIRI

 

WANANCHI -SHINYANGA WALALAMIKA KUPANDA KWA NAULI ZA VYOMBO VYA USAFIRI



                              NA HALIMA KHOYA, SHINYANGA

BAADHI ya abiria Mkoani Shinyanga wamelalamikia kupanda kwa nauli za mabasi hali iliyosababishwa na kupanda kwa bei za kununulia mafuta pia mawakala kutoa tiketi zisizo rasmi kinyume cha sheria iliyopo sasa.

Wakizungumza na Shinyanga Blog leo agosti 29,2022 baadhi ya abiria wamedai wakati huu ni kuanza kuwadhibiti mawakala wanaoenda kinyume huku wakiiomba Serikali kutowafumbia macho wanaokwenda kinyume .

Wamesema kuwa kupanda kwa nauli kunawagharimu kwasababu ya mabadiliko hayo jambo linalopelekea kukosekana kwa uaminifu kati ya abiria na mawakala na kueleza kuwa kumekua na vitendo visivyostahili ambavyo vinafanywa na baadhi ya mawakala ikiwa ni pamoja na kutumia lugha mbaya kwa wateja wao.

Mmoja wa mawakala wa mabasi aliyepo stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani Abubakar Khamis, amekiri kupanda kwa nauli hizo hali iliyosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta na kuwataka abiria hao kuacha kukata tiketi kwa mawakala bali waende katika ofisi za gari husika ili kukatiwa tiketi kwa njia ya mtandao.

Katibu wa umoja wa mawakala Stendi kuu ya mabasi Suleiman Mohamed amewataka abiria hao kujali usalama wao kwa kukataa kupanda katika mabasi ambayo hakuna siti zilizokuwa wazi ili kutekeleza ilani ya usalama wa barabarani.

Kaimu Afisa Mfawidhi Mamlaka ya usafirishaji aridhini Mkoa Shinyanga (LATRA),Denis Magembe amebainisha kuwa, licha ya utolewaji wa elimu kwa watoa huduma pamoja na abiria hao bado kumekua na tatizo hilo kwani mtoa huduma yeyote atakae zidisha abiria sheria zipo.

"Kwa mujibu wa kanuni za usafirishaji wa mabasi ya abiria kwa mwaka 2020/22 kifungu no.22 mtoa huduma yeyote atakae gundulika kwa kuzidisha abiria atachukuliwa hatua na faini yake ni sh 250,000"amesema magembe.

Magembe amesema kuwa elimu inaendelea kutolewa nakuwakumbusha wamiliki wa mabasi kuwa ifikapo tarehe 1/09/2022 wahakikishe wanatoa risiti kwa abira kwa njia ya mtandao.


.

Post a Comment

0 Comments