Header Ads Widget

TAKUKURU SHINYANGA YABAINI MADUDU MIRADI YA MAENDELEO FEDHA ZA UVIKO-19 YENYE THAMANI YA BILIONI 13.7

 Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Shinyanga Donasian Kessy akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya utendaji kazi kipindi cha robo nne ya mwaka wa fedha (2021/2022) kipindi cha kuanzia April hadi Juni.


Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Shinyanga Donasian Kessy akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya utendaji kazi kipindi cha robo nne ya mwaka wa fedha (2021/2022) kipindi cha kuanzia April hadi Juni.

Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Shinyanga Donasian Kessy akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya utendaji kazi kipindi cha robo nne ya mwaka wa fedha (2021/2022) kipindi cha kuanzia April hadi Juni.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Shinyanga imebainisha jumla ya miradi ya maendeleo 17 itokanayo na fedha za UVIKO-19 mkoani humo imekutwa na dosari kwa kutekelezwa chini ya kiwango.


Mkuu wa Takukuru mkoani Shinyanga Donasian Kessy, amebainisha hayo jana wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha robo nne ya mwaka wa fedha (2021/2022) kuanzia April hadi Juni.

Amesema Taasisi hiyo kwa kpindi hicho ilijikita katika uzuiaji Rushwa, na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoani humo, pamoja na kutoa elimu kwa jamii pamoja na wanafunzi juu ya utoaji taarifa wa vitendo vya Rushwa.

“Katika eneo za uzuiaji Rushwa, Takukuru Shinyanga tulifanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo 17 itokanayo na fedha za UVIKO-19 yenye thamani ya Sh.bilioni 13.7 na kubaini dosari kwenye miradi hiyo,” amesema Kessy.

“Miradi tulioitembelea ilihusu Sekta ya Ujenzi, Elimu, Maji, Afya na Utawala, Miradi hii yote inajumuisha Miradi ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano ya UVIKO-19, na Miradi Minne kati ya 17 ndiyo imebainika kuwa na Dosari,” ameongeza.

Aidha, ametaja dosari ambazo wamezikuta kwenye utekelezaji wa Miradi hiyo ya maendeleo itokanayo na fedha za UVIKO-19 kuwa ni ukuta kutonyooka katika ujenzi wa vyumba vya Madarasa, Madirisha ya Alluminium kutofit, Milango, pamoja na Chemba za Majitaka kuwa chini ya kiwango na kuangiza jenzi hizo zifanyiwe Maboresho.

Amesema pia kwa kipindi hicho wamefanya uchambuzi wa mifumo kuhusiana na changamoto za ujenzi wa vyumba vya Madarasa kupitia fedha hizo za UVIKO-19 na uendeshaji wa jumuiya za watumiaji wa maji ngazi ya jamii, na kubaini kuwepo na Dosari ya zinazoweza kupelekea uwepo mianya ya Rushwa.

Anaongeza kuwa katika dawati la uchunguzi wamepokea taarifa 29 za malalamiko, ambapo 23 zilihusu Rushwa, Serikali za Mitaa Nane, Ujenzi Sita, Polisi Tatu, Maji Mbili, Elimu Mbili, Biashara Mmoja, Afya Mmoja, na taarifa 18 uchunguzi wake unaendelea, Tano uchunguzi umekamilika, kesi Saba zinaendelea Mahakamani.

Amefafanua kuwa pia walikuwa na kesi 10 ambazo zilikuwa zikiendelea Mahakamani, kesi Saba walishinda Mahakamani na watuhumiwa kutiwa hatiani na kulipa faini, huku mtuhumiwa mmoja akishindwa kulipa faini na hatimaye kufungwa Jela miaka mitatu.

Katika hatua nyingine amesema wameendesha semina mbalimbali na kutoa elimu ya mapambano ya kupinga Rushwa, kwa Skauti, kwenye mikusanyiko wa wananchi, kuimarisha Klabu za wapinga Rushwa Shule za Msingi, Sekondari na vyuoni.

Amesema pia wameendesha kampeni ya ‘vunja ukimya kata Rushwa ya ngono’ katika vyuo vitatu mkoani Shinyanga ambavyo ni Veta, Ushirika na chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija, na kubaini kuwepo na viashiria vya Rushwa kwa Wahadhiri kwa kufelisha makusudi wanafunzi ili wafanye nao ngono.

Kessy ametoa wito kwa wananchi mkoani Shinyanga pamoja na wanafunzi, kuendelea kutoa taarifa juu ya vitendo vya Rushwa ambavyo vimekuwa vikiwanyima kupata haki zao, kwa kupiga simu namba 0738-150196 au 0738-15019, Ofisi ya Kahama 0738-150198.

Post a Comment

0 Comments