Header Ads Widget

SHIRECU YAPUNGUZA DENI WALILOKUWA WAKIDAIWA NA BENKI YA TIB WAANZISHA MIKAKATI MIPYA.Wajumbe wa mkutano mkuu kutoka chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga {Shirecu}

Na Suzy Butondo

HATIMAYE  Chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) kimepunguza deni lililokuwa likidaiwa na benki ya uwekezaji (TIB) ambalo lilikuwa ni deni la Sh Bilioni 15,8 na kubaki ikidaiwa kiasi cha Sh Billioni sita ambayo itaendelea kulipa kwa kila mwezi.


Hayo yamesemwa jana kwenye mkutano maalumu wa kawaida wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa Shirecu ambao uliitishwa kwa lengo la kuwasilisha deni jipya la TIB lililobaki baada ya mgawanyo wa vyama vikuu vya ushirika vitatu, ikiwa ni pamoja na kupitisha bajeti ya nyongeza na kufufua viwanda.

Akizungumza kwenye mkutano huo mwenyekiti wa Chama cha ushirika Shirecu Kwiyolecha Nkilijiwa amesema deni lilikuwa ni kubwa sana lakini watakuwa wakilima kiasi cha sh 4,170'000 kwa kila mwezi

"Leo kazi iliyokuwepo kwa wanachama ni kulipokea deni jipya lililobaki badala ya sh Bilioni 15 sasa ni sh 6 bilioni, na hii ndiyo ajenda kuu iliyosababibisha ufanyike mkutano huu wa mwaka pamoja na kupitisha nyongeza ya bajeti "amesema Nkilijiwa.

Nkilijiwa amesema wanachama pia wamekubaliana kupitisha bajeti ya nyongeza ambayo ilitokana na bajeti kuu ya kwenye mkutano mkuu, ambayo ilienda ikakokotolewa ikaonekana kuna faida inayobaki,

Nkilijiwa ameongeza "Nawashukuru wanachama wangu kwa kuyapitisha haya, hivyo tunaamini tutakapofufua viwanda vyetu ambavyo vitakuwa vya kukamua mafuta tutafanya biashara na tutalipa madeni yetu kwa wakati, na mpango mkakati wetu ni kulipa wadai wote wanaoidai shirecu

Mjumbe mteuliwa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Maligisa Doto amesema wamejipanga kuanzisha vyanzo vingine vya mapato zaidi ili waendelee kulipa madeni kwa wadai wote wanaoidai shirecu ikiwemo ufugaji wa nyuki na kilimo ikiambatana na kuwa na trecta ambalo litasaidia kwenye shughuli ya kilimo ili kuongeza mapato.

Makamo mwenyekiti wa Shirecu Josephate Limbe, amesema lengo la chama hicho ni kuhakikisha hawadhalishi deni lolote,pia wameridhia kulipa sh 4 milioni kwa kila mwezi na wataongeza udhalishaji wa ndani ilikupunguza madeni yaliyopo.

"Tunawashukuru wajumbe wote kwa kukubaliana kwa pamoja kupitisha bajeti ya nyongeza nakulipokea deni la nyongeza lililobaki hivyo tunaamini tutaendelea kufanya vizuri zaidi .

Mmoja wa wanachama hao Jabai Madereke amesema wamepitisha bajeti ya nyongeza ili waweze kupunguza madeni kwa wafanyakazi na kwa wastaafu ambao bado wanadai, lakini pia kufufua baadhi ya viwanda vilivyokuwa havifanyi kazi ili kujiongezea mapat
Mwenyekiti wa mktano mkuu wa muda Wilson Mashishanga.

Mjumbe wa kikao maalum aliyechaguliwa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Maligisa Doto.Mwenyekiti wa Shirecu Kwiyolecha Nkilijiwa.Makamu mwenyekiti wa Shirecu Joesph Limbe.

TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807