Header Ads Widget

MBUNGE KAPINGA AWATAKA UVCCM KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO YA HALMASHAURI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Mbunge Viti Maalum kundi la vijana Taifa Judith Kapinga, akizungumza na Viongozi wa UVCCM.

Suzy Luhende,Shinyanga

Mbunge viti maalum kundi la vijana Taifa Judith Kapinga amewataka Wenyeviti wa Uvccm Kata wilaya ya Shinyanga mjini, kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na halmashauri, ili kuhakikisha vijana wote wa chama cha Mapinduzi (UVCCM) wanajishughulisha na shughuli za kimaendeleo na kujikwamua kiuchumi.

Amebainisha hayo leo Agost Mosi mwaka huu, wakati akizungumza na viongozi wa Uvccm wilaya ya Shinyanga mjini,ambapo amesema vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) hawapaswi kulia na njaa, bali wenyeviti wa Uvccm kata wanatakiwa kuchangamkia fursa za mikopo ya halmashauri ili kuhakikisha vijana wanafanya shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato.

Kapinga amesema vijana wanatakiwa wawe vijana wa kisasa wasikae wanasema wanakipenda Chama tu huku wakilia njaa, wanatakiwa kuchangamkia fursa za mikopo yenye tija ili kuisaidia serikali kwa sababu haiwezi kuajili vijana wote.

"Tunatakiwa tuwe vijana wa kisasa tusikae tu tukisema tunakipenda chama, tukipende na tuchangamkie fursa za mikopo inayotolewa na halmashauri, ni aibu mwenyekiti wa kata kuona vijana wako wanalia na njaa huku fursa za kifedha zikiwepo"amesema Kapinga.

"Nimetembelea kiwanda cha vijana cha kutengeneza Chark, pia nimetembelea kiwanda cha kutengeneza magodoro na vikundi vinavyojishughulisha na kilimo cha mahindi matunda na mbogamboga kilichpo katika kata ya Lubaga, nawapongeza sana kwa juhudi mnazozifanya nimeona mnapenda sana kazi vijana wa Shinyanga"amesema Kapinga.

Aidha aliwataka vijana wa Uvccm wilaya ya Shinyanga mjini walinde afya zao, ili chama kiweze kuimalika zaidi, kwani kuna maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yameongezeka, hivyo amewataka watumie kinga, kama si lazima wasubiri ili kuwa na vijana wenye afya bora.

"Hatuwezi kuwa na vijana ambao hawatunzi afya zao, tunatakiwa tuwe na vijana shupavu wenye afya njema, pia kijana wa CCM anatakiwa kuwa na maadili na kiongozi lazima uwe wa mfano kwa vijana wengine acha kuendekeza mitulinga (pombe) kunywa kwa ustaarabu, nimeyasema haya kwa sababu ulevi ni changamoto kwa vijana wengi"amesema Kapinga.

"Ukiwa mwenyekiti ubebe uenyekiti wako na ukiwa katibu ubebe ukatibu wako, tunachangamoto ya maadili katika nchi yetu, kwani takwimu zinaonyesha watoto wa kiume wengi wanafanyiwa ukatili wa kulawitiwa zaidi, hivyo tuwe mfano tuelimishe jamii iondokane na ukatili huu"amesema Kapinga.

Kwa upande wake katibu wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Ally Majeshi amewataka viongozi waliochaguliwa wasitumike vibaya, badala yake watumike ndani ya chama cha mapinduzi CCM, kwani makundi yaliyokuwepo kwenye uchaguzi wa vijana yameisha kama kuna mtu amewasaidia mahali sasa ni viongozi wa CCM, hivyo watapiga kura kwa utashi wao wasiwe viongozi wa kufuata mikumbo.

Katibu wa Uvccm wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Faraj Katalambula amesema asilimia nne ya halmashauri imenufaisha vikundi vingi vya vjiana sambamba na asilimia hiyo pia kuna makundi mbalimbali, kundi la hamasa wameanzisha shughuli zao na vijana baraza la jumuia nayo inashughuli zake za kimaendeleo.

Mwenyekiti wa Uvccm mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge amesema anaishukuru serikali kwa kutoa mikopo kwa vijana ambao umetembelewa na mbunge viti maalum Taifa Kapinga mradi wa chark wa Sh 24 milioni, mradi wa kutengeneza Magodoro wa Sh 40 milioni uliopo kata yamjini na mradi wa shamba la heka saba wa Sh 100 milioni, uliopo kata ya Lubaga.

Mbunge Viti Maalum kundi la vijana Taifa Judith Kapinga, akizungumza na Viongozi wa UVCCM.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akizungumza kwenye mkutano huo.

Katibu wa Uvccm wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Faraj Katalambula, akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mbunge Viti Maalum kundi la vijana Taifa Judith Kapinga, akiangalia uzalishaji wa Chaki

Mbunge Viti Maalum kundi la vijana Taifa Judith Kapinga, akiwa kwenye shamba la Ujasiriamali Lubaga.

Mbunge Viti Maalum kundi la vijana Taifa Judith Kapinga, akiwa kwenye shamba la Ujasiriamali Lubaga.

Post a Comment

0 Comments