Header Ads Widget

KONGAMANO LA AFRIKA MRADI WA KUZUIA VITENDO VYA KUJIUA LAFANYIKA NCHINI RWANDA

Washiriki wakiwa kwenye  mafunzo.
Mkufunzi Mkuu Rev. Jerry Vreeman akitoa mafunzo ya Uongozi kwa Washiriki 60.
Mwakilishi kutoka Tanzania mkoani Shinyanga John Eddy akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo

Kongamano la Kimataifa la Afrika la Mradi wa kuzuia vitendo vya kujiua (Africa Project Against Suicide - APAS) limefanyika kwa muda wa siku tatu (July 28-30) Kigali, Rwanda.

 
Kongamano hilo limejumuisha nchi 19 za Afrika, nchi ya Marekani na Uingereza. Kongamano hilo lilikuwa na lengo la kutoa mafunzo ya uongozi juu ya namna ya kuzuia vitendo vya kujiua (suicide) kwa kutoa tumaini (Hope) kwa wanaofikia hatua ya kuona kwamba kujiua ni suluhisho.

Mkufunzi Mkuu kutoka nchini Marekani katika Taasisi ya L. I.O.N (Leadership In Obscurity Network) Jerry Vreeman amewaasa washiriki kuwa Viongozi wanaotoa tumaini kwa watu wanaowatumikia.

"Mnaporejea katika Mataifa yenu, mkawe chachu na tumaini kwa waliokata tamaa na kujiona hawana thamani au sababu ya kuishi. Mkae nao karibu sana (Be there), muwaoneshe mustakabali mzuri ulioko mbele yao na giza ambalo wanaweza kusababisha kama watakuwa wanafikiria kujidhuru" Alisema Vreeman.

Kwa upande wake Mratibu wa APAS kutoka Afrika na Mwakilishi wa Mratibu Mkuu Rev. Honey Olawale amewatia moyo washiriki kutokata tamaa mbali ya changamoto wanazokabiliana nazo katika utendaji wao. Baada ya mafunzo hayo kila nchi Mshiriki iliwasilisha mkakati wake.

Nchi ya Tanzania iliwakilishwa na Shirika la Right To Life la mkoani Shinyanga.

Nchi 19 ambazo ziliweza kushiriki kongamano na mafunzo ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Afrika ya Kusini, Togo, Benin, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Lesotho, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Senegal, Ghana, Nigeria, Ivory Coast, Marekani na Uingereza.

Lengo kubwa la APAS ni kuunganisha jitihada za Wadau na Jamii ili kujenga Afrika iliyo huru dhidi ya Vitendo vya kujiua (Suicide) kwa kujikita kwenye Afya ya akili, malezi na matumaini.

Post a Comment

0 Comments