Header Ads Widget

KATAMBI AHAMASISHA WANANCHI WASHIRIKI KIKAMILIFU KUHESABIWA SENSA KESHO, AKEMEA SIASA ZA MAJUNGU

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, akiwa ameshika bango lenye picha ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwasili kwenye Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga, kuhamasisha wananchi wajitokeze kesho kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, akizungumza na viongozi wa CCM, na Kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi hapo kesho.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi, amewasisitiza wananchi wa Shinyanga, wajitokeze kwa wingi siku ya kesho kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi.

Kesho Agosti 23, 2022 ni siku ya kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi hapa nchini, ambapo wananchi watahesabiwa na Serikali kupata idadi ya watu wake kamili kwa kila eneo.

Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, amebainisha hayo leo Agost 22, 2022 wakati wa kikao chake na viongozi wapya wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Kata na Jumuiya zake, ambao walichaguliwa kwenye uchaguzi wa ndani wa Chama hicho.

Amesema zoezi la kuhesabiwa Sensa ni muhimu sana kwa Maendeleo ya nchi, ambapo Serikali ikiwa na idadi kamili ya watu wake, itasaidia katika Mipango yake ya kuwatekelezea mahitaji yao kulingana na idadi yao.

"Sensa ni Maji, Elimu, Barabara, Umeme,Vituo vya Afya na mambo mengi tu ya maendeleo, hivyo nawasihi wananchi wa Shinyanga mjitokeze kwa wingi kuhesabiwa kesho Sensa ya watu na Makazi ni faida yetu kimaendeleo," amesema Katambi.

Aidha, amewataka viongozi hao wakahamasishe wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa.

Katika hatua nyingine Katambi, amewataka viongozi washikamane, kupendana, na kuacha majungu na kuchongeana hovyo kwa kufanya siasa za fitina ambazo zinakwamisha Maendeleo.

Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Ally Shabani Ally, amewasihi wananchi wajitokeze kuhesabiwa ili zoezi hilo lifanikiwe kwa asilimia 100.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, akizungumza na viongozi wa CCM, na Kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi hapo kesho.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, akizungumza na viongozi wa CCM, na Kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi hapo kesho.

Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Ally Shabani Ally akizungumza kwenye mkutano huo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Said Bwanga akizungumza kwenye mkutano huo.

Viongozi wapya wa CCM Ngazi ya Kata na Jumuiya zake wakiwa kwenye Mkutano huo.

Viongozi wapya wa CCM Ngazi ya Kata na Jumuiya zake wakiwa kwenye Mkutano huo.

Viongozi wapya wa CCM Ngazi ya Kata na Jumuiya zake wakiwa kwenye Mkutano huo.

Viongozi wapya wa CCM Ngazi ya Kata na Jumuiya zake wakiwa kwenye Mkutano huo.

Viongozi wapya wa CCM Ngazi ya Kata na Jumuiya zake wakiwa kwenye Mkutano huo.

Viongozi wapya wa CCM Ngazi ya Kata na Jumuiya zake wakiwa kwenye Mkutano huo.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, akiwa ameshika bango lenye picha ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwasili kwenye Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga, kuhamasisha wananchi wajitokeze kesho kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi.

Post a Comment

0 Comments