Header Ads Widget

HALMASHAURI YA USHETU IMEJIVUNIA KUONGEZA MAPATO YA NDANI KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA.

Madiwani wa halmashauri ya Ushetu wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani.

Na Kareny Masasy

HALMASHAURI ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga imejivunia kuongeza mapato ya ndani kutoka asilimia 67 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 hadi kufikia asilimia 83 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Hayo yamesemwa jana na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Gagi Lala kwenye Kikao cha robo ya nne ya mwaka chenye lengo la kujadili uwajibikaji na utekelezaji wa miradi kwa kipindi cha mwaka mmoja sambamba na uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo.

Mwenyekiti Lala amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja mabadiliko yamefanyika na matokeo yake ni makubwa hakuna budi kujipongeza pia serikali awamu ya sita iliyoleta fedha nakutekeleza miradi mbalimbali.

Diwani wa kata ya Ulowa Gabriela Kimaro amepongeza kwa taarifa iliyosomwa na ofisa mipango Theresia Nsumba iliyoeleza kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wamepokea kiasi cha zaidi ya sh Billioni 10 fedha ambazo kutoka serikali kuu,mapato ya ndani ya halmashauri na wafadhili.

Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye ni diwani wa kata ya Sabasabini Emanuel Makashi amesema kuwa kazi aliyoifanya ni nzuri uongozi ni kuachiana na atatoa ushirikiano katika uongozi uliopo ili waendelee kusonga mbele.

Doa Limbu ameshukuru kuchaguliwa kwa kupigiwa kura na madiwani wote 27 huku akieleza kuboresha zaidi mahusiano kati ya madiwani na wataalamu.

Diwani Limbu amesema kuwa katika uzoefu wake kwenye udiwani amegundua halmashauri kuwa na vigezo nakuvifuata ili kuendelea kupata hati safi.

‘Vinavyohitajika hasa ni kukusanya mapato, kujibu hoja za mkaguzi wa hesabu na kutenga asilimia 10 zinazohitajika kutoka mapato ya ndani kwa kuwafikia walengwa”amesema Limbu.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Linno Mwageni ametaka wananchi washirikishwe katika miradi ili fedha zilizotengwa kutekelezwa ziweze kutosha kukamilisha miradi walioianzisha.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Gagi Lala ambaye ni diwani wa kata ya Igwamanoni akifungua kikao cha robo ya nne ya mwaka katika kujadili uwajibikaji na utekelezaji wa maendeleo kwa kipindi cha mwaka mmjoa.
Diwani wa kata ya Nyankede Doa Limbu akiongea kwa kujinadi kuomba kura kabla ya kuchaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu.

Diwani wa kata ya Nyankende Doa Limbu akijipigia kura kwa nafasi aliyogombea ya makamu mwenyekiti wa halmashauri ya ushetu.


Post a Comment

0 Comments