Header Ads Widget

AKINA MAMA MSALALA WAPEWA ELIMU YA UNYONYESHAJI WATOTO


Afisa lishe wa halmashauri ya Msalala Peter Shimba akitoa elimu ya unyonyeshaji wa wazazi waliofika Zahanati ya kijiji Cha Segese katika siku ya maadhimisho ya unyonyeshaji duniani.

Akina mama wakipewa elimu ya unyonyeshaji.

Na Kareny Masasy, Msalala.

WAZAZI halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwanyonyesha watoto wao hadi watakapo fikisha umri wa miaka miwili ili kuweza kuujenga ubongo na afya ya mwili.

 
Afisa lishe wa halmashauri Peter Shimba amesema hayo Leo tarehe 8/8/2022 katika kuhitimisha siku ya unyonyeshaji iliyofanyika kwenye Zahanati ya Segese huku akieleza kuwa unyonyeshaji maziwa ya mama pekee kipindi Cha miezi sita ni asilimia 99.

Shimba amesema kuwa mtoto anajengwa ubongo wake ndani ya siku 1000 yaani miaka miwili mama anapomnyonyesha kikamilifu anaujenga vizuri ubongo wa mtoto hivyo wasiachishe mapema kuwanyonyesha.

Ofisa lishe mkoa wa Shinyanga Denis Madeleka amesema kuwa mkoa wa Shinyanga una asilimia 83 ya unyonyeshaji maziwa ya mama pekee kwa kipindi Cha miezi sita.

Madeleka amesema kuwa watoto wanaoendelea kunyonya baada ya mwaka mmoja ni asilimia 78 na wanaonyonyesha baada ya miaka miwili ni asilimia 27.9.

Kwa mujibu wa taasisi ya chakula na lishe (TNFC ) inaeleza kuwa kwa tafiti zilizofanywa na wataalamu walibainisha kuwa maziwa ya mama yanauwezo mkubwa wa kupunguza vifo vya watoto wachanga na wadogo.

Post a Comment

0 Comments