Header Ads Widget

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUMALIZA KUHESABIWA SENSA KAHAMA

Afariki dunia muda mchache baada ya kuhesabiwa

Hospitali ya Kahama, mkoani Shinyanga 

 Na kareny Masasy, KAHAMA

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa Kata ya Majengo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga amefariki dunia saa chache baada ya kuhesabiwa na makarani wa sensa nyakati za usiku katika hospitali ya Manispaa ya Kahama.

 
Pia mtu mwingine aliyekuwa amelazwa wodini katika hospitali hiyo alikataa kuhesabiwa mpaka awaone viongozi wa eneo lake.

Akiongea na Waandishi wa habari, Karani wa Sensa aliyefanya zoezi hilo hospitalini hapo Robert Mayunga amesema kuwa zoezi limeenda vizuri kwani walianza majira ya saa sita usiku kwa kuanzia hospitalini hapo.

Mayunga amesema kuwa mgonjwa aliyekuwa akikataa kuhesabiwa tayari ameshahesabiwa baada ya kupata maelezo na kujiridhisha na zoezi zima. Vilevile amesema, Mzee aliyefariki alikuwa na kijana wake aliyetambulishwa kwa jina la Williams Shija ambaye pia alitoa maelezo kabla mzee hajafariki dunia.

Post a Comment

0 Comments