Header Ads Widget

WASABATO KAHAMA WAPEWA SOMO LA LISHE KWA WAJAWAZITO

Kaimu Ofisa lishe halmashauri ya Msalala Peter Shimba akitoa elimu ya lishe Kanisani

Waumini wakiwa Kanisani.

Waumini wakiwa Kanisani.

Na Kareny Masasy, KAHAMA

WAUMINI wa Kanisa la Wadventista Wasabato Kahama mkoani Shinyanga, wameshauriwa kuwapatia wajawazito na watoto lishe yenye mlo kamili kuweza kupata virutubisho mwilini ili kuepukana na changamoto ya upungufu wa damu pamoja na udumavu.

Kaimu ofisa Lishe kutoka halmashauri ya Msalala Peter Shimba amesema hayo Julai 23,2022 mbele ya waumini wa Kanisa hilo katika ujifunzaji wa somo la afya kanisani hapo huku akiwaeleza kuwa kundi la watoto chini ya umri wa miaka mitano ndiyo linaloongaza kwa upungufu wa damu.

Shimba amesema kuwa wapo wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano ambao wamekuwa hawafuati ulaji unaofaa yaani chakula chenye mchanganyiko na wenye kufuata makundi matano ya vyakula ndiyo tatizo linalowakumba la udumavu.

“Wazazi na walezi 156 kwa leo nimewapatiwa elimu juu ya chakula na lishe kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na wajawazito na watoto wenye udumavu tumefanikisha kuwatibu walikuwa na dalili za ngozi inabonyea,wakati mwingine kutoa majimaji,mashavu na tumbo kuvimba “alisema Shimba.

Shimba amesema kuwa kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Tanzania Demographic Healthy Survey (THDS)mwaka 2018 mkoa wa Shinyanga una udumavu asilimia 32.1 na upungufu wa damu kwa watoto chini ya umri wa miaka tano ni asilimia 12.3.

“Tunatakiwa kuwekeza zaidi kwa watoto tangu umri 0 hadi siku 1000 katika lishe kwani ndipo kipindi ubongo wa mtoto unavyoanza kukua vizuri kiakili na kutowekeza hasa shuleni wakati akiwa na umri mkubwa huku ukilalamika mtoto huyu hana akili kumbe ni kosa la mzazi” alisema Shimba.
 
Mwinjilisti kutoka Kanisa hilo Alfred Ezeckiel amsema kuwa waumini wapende kusoma vitabu mbalimbali kwani hata katika maandiko ya vitabu vya kiroho lishe bora kwa mwili wa binadamu imeandikwa pia ukifuatilia masuala ya afya utajua vitu vingi na kuikomboa familia yako.

Baadhi ya waumini wa Kanisa hilo akiwemo Aghata Boniface na Jonh Alloyce walisema kuwa wanao ufahamu juu ya lishe kwa kipengele cha virutubisho mwilini ambavyo ni vitu vinavyokwenda kujenga mwili na utapiamlo kupata chakula bila kuzintaia mahitaji ya mwilini.

Post a Comment

0 Comments